Dube wa Azam FC kupelekwa Afrika Kusini kwa matibabu

Mshambuliaji Mzimbabwe wa Azam FC, Prince Dube Mpumelelo aliyeumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Yanga SC janA Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam anatarajiwa kwenda Afrika Kusini kwa matibabu zaidi, anaripoti Mwandishi Diramakini.Kwa mujibu wa taarifa ya Azam FC iliyotolewa leo Novemba 26,2020 imesema kwamba Dube mwenye umri wa miaka 23,jana Novemba 25, 2020 aliumia dakika ya 15 kwa kuvunjika mfupa wa mbele wa mkono wake wa kushoto uitwao Ulnar, unaoanzia kwenye kiwiko na kushuka hadi kwenye kidole cha mwisho. 

Taarifa hiyo imesema kwamba Dube ataondoka nchini Jumapili ya Novemba 29, mwaka huu kwa ndege ya Shirika la Kenya Airways (KQ) na atatibiwa kwenye Hospitali ya Vincent Pallotti iliyopo Cape Town, chini ya daktari bingwa wa mifupa, Robert Nicolas.

"Azam FC tumekuwa tukiitumia hospitali hii kutibia wachezaji wetu tangu mwaka 2011.
Tunampa pole na kumtakia matibabu mema na kupona haraka, Prince Dube,"imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news