Ngumi kuruhusiwa Zanzibar? Mwakinyo ana jambo

Bondia wa Kimataifa nchini Tanzania, Hassan Mwakinyo amewasili visiwani Zanzibar kwa ajili ya kuiomba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iweze kuruhusu mchezo wa ngumi visiwani humo, anaripoti Mwandishi Diramakini.

“Zanzibar kuna vipaji vingi sana hapa, lakini hawapati nafasi ya kuonyesha vipaji vyao, kama Zanzibar wataruhusu mchezo huu basi Zanzibar itatoa Mbondia wakubwa na wa Kimataifa,”amesema Mwakinyo. Mwakinyo ameongeza kuwa, amefurahi sana kufika Zanzibar na Zanzibar ni moja ya sehemu ambayo anaipenda. Mratibu wa Hassan Mwakinyo ambaye ni Ahmada Salum Suleiman amesema kuwa,lengo la Mwakinyo kuja Zanzibar ni kuukuza utalii wa ndani na kuutangaza kimataifa ili wageni wavijue vivutio vya Zanzibar.

Pia wajue kama Zanzibar hakuna Corona na pia Mwakinyo amekuja kuweza kufafanua na kuiomba Serikali ya Zanzibar kurejesha mchezo wa ngumi. Mwakinyo atakuwepo Zanzibar kwa siku mbili na atatembelea vituo mbalimbali vya habari vya Zanzibar ikiwemo vivutio vya utalii vya Mjini ikiwemo kukutana na viongozi wa Serikali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news