Dkt.Ngailo awaondoa wasiwasi wakulima upatikanaji wa mbolea Mbeya

Wakulima mkoani Mbeya watakiwa kuondoa wasiwasi kuhusu upatikanaji wa Mbolea Mkoani humo na kuwa waendele na maandalizi ya mashamba yao ili kwendana na msimu huu wa kilimo nchini, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Hayo yamesemwa na Mtendaji wa Mamlaka ya Mbolea Tanzania, Dkt. Stephan Ngailo katika ziara yake kwa lengo la kujionea hali ya upatikanaji na usambaziji wa mbolea nchini ili kuhakikisha inakidhi mahitaji ya wakulima kwenye mikoa yote inayojishughulisha na kilomo cha mazao mbalimbali ya chakula na biashara.


Pichani juu na chini ni Mkurugenzi, Mtendaji wa Mamlaka ya Mbolea Tamzania Dkt . Stephan Ngailo akikagua uwepo wa mbolea katika maghala mbalimbali ya mbolea katika Mkoa wa Mbeya wakati wakulima wapo katika maandalizi ya msimu wa kilimo. Amewatoa wasiwasi wakulima kuwa mbolea za aina zote zipo waendelee na maandalizi ya kilimo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt.Stephan Ngailo akipewa maelezo kutoka kwa Afisa wa Kampuni la Eka Moja Ltd linalotoa mikopo ya mbolea kwa wakulima katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi.

Dkt.Ngailo amesema kuwa, ameridhishwa na uwepo wa mbolea ya kutosha kwenye Maghala mbalimbali yaliyopo mkoani Mbeya, huku akiwapongeza wafanyabiashara ya bidhaa hiyo kwa kufuata sheria na taratibu zote zilizowekwa na Serikali pamoja na kutoa mikopo ya mbolea kwa zaidi ya wakulima 25,000 pia amekerwa na wafanyabiashara wachache wanaokiuka taratibu zilizopo.

“Nimefika Mbalizi, Chunya na hapa Mbeya, nimeridhishwa sana na uwepo wa mbolea ya kutosha, pia nimeridhishwa sana na uadilifu wa wafanyabiashara ya mbolea hapa Mbeya wanafanya kazi nzuri sana, ila nimekerwa sana na wafanyabiashara wachahe, wanaokiuka utaratibu kwa kufungua mifuko ya mbolea na kuuza kwa kupima, hawa tutawashughulikia,"amesema Dkt.Ngailo.

Wafanyakazi wa moja ya maghala ya mbolea mkoani Songwe wakishusha mbolea kwenye gari na kuhifadhi katika ghala hilo tayari kwa kuwauzua wakulima wakati huu wa msimu wa kilimo.
Pichani ni sehemu ya shehena ya mbolea iliyohifadhiwa kwenye moja ya maghala mkoani Mbeya.

Ili kuongeza tija kwenye kilimo, Dkt.Ngailo amewashauri wakulima kuzingatia kanuni za kilimo bora ambacho ni pamoja na kuchagua eneo sahihi, kupanda kwa wakati, kupanda mbegu kwa usahihi pamoja na kuweka mbolea kwa husahihi na wakati sahihi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini (TFRA), Dkt.Stephan Ngailo anaendelea na ziara yake ya kukagua na kujionea hali ya upatikanaji na usambaziji wa mbolea nchini kwenye mikoa ya Songwe, Katavi, Rukwa, Kigoma na Tabora.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news