Ni Mukoko Tonombe, Cedric Kaze Tuzo za VPL

Mukoko Tonombe kutoka Klabu ya Yanga amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2020/21 huku kocha wake Cedric Kaze naye akichukua tuzo ya kocha bora. Tuzo hizo wamezitwaa baada ya kuwashinda wenzao walioingia nao fainali katika uchambuzi uliofanywa jijini Dar es Salaam wiki hii.

Uchambuzi uliofanywa na Kamati ya Tuzo ya VPL inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Oktoba, Yanga ilicheza mechi nne na kushinda zote jambo lililowawezesha kupand kutoka nafasi ya tatu hadi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom inayoshirikisha timu 18.

Ni kwa kuifunga Coastal Union 3-0, Polisi Tanzania 1-0, KMC 1-2 na Biashara United 0-1 huku Mukoko akitajwa kutoa mchango mkubwa katika ushindi huo ikiwa ni pamoja na kufunga bao moja dhidi ya Polisi Tanzania.

Mukoko amewashinda washambuliaji wa Azam FC, Prince Dube na mshambuliaji wa Gwambina FC, Meshack Abraham aliongia nao fainali.

Dube aliiongoza Azam FC kubaki kileleni baada ya kuvuna alama 10 mwezi Oktoba, ikishinda tatu, sare moja na kupoteza moja, huku mshambuliaji huyo akifunga mabao matatu na kutoa pasi tatu za usaidizi wa mabao.

Kwa upande wake, Meshack aliiongoza Gwambina FC kupata alama nane ikishinda michezo miwili, sare miwili na kupoteza mmoja, ikipanda kutoka nafasi ya 17 hadi ya 14 akiifungia timu yake mabao manne.

Naye Kaze amewashinda Aristica Cioaba wa Azam FC na Francis Baraza wa Biashara United FC ambapo Kaze aliiongoza Yanga katika michezo mitatu na kushinda yote. Yanga chini ya Kaze ilizifunga Polisi Tanzania, KMC na Biashara United na kupanda kutoka nafasi ya tatu hadi ya pili.

Cioaba aliiongoza Azam kushinda michezo mitatu, sare moja na kupoteza moja, huku Baraza akiiongoza Biashara kushinda michezo mitatu na kupoteza miwili ikipanda kutoka nafasi ya saba hadi ya nne katika Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. (anaripoti Mwandishi Diramakini).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news