Taifa Stars yashindwa kung'ara kwa Tunisia

Licha ya matarajio makubwa ya Watanzania juu ya ushindi kwa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, matokeo yamejiri ndivyo sivyo, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Ni baada ya mechi hiyo Timu ya Tunisia kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) 2022 nchini Cameroon uliopigwa uwanja wa Stade des Olympiakus kuifunga Taifa Stars 1-0.

Bao pekee la ushindi kwa Tunisia, kwenye mchezo wa kundi J uliochezwa Novemba 13, 2020 limefungwa na Youssel Msakni 18' kwa mkwaju wa penalti.

Aidha, jitihada za Taifa Stars kupata bao hazijaweza kuzaa matunda hadi dakika tisini zinakamilika ambapo Simon Msuva na Bakari Mwamnyeto walionyeshwa kadi ya njano kwenye mchezo huo.

Mchezo ambao Tunisia waliutawala kwa kiasi kikubwa eneo la kiungo na ushambuliaji huku Aishi Manula akifanya kazi ya ziada kuokoa michomo minne ya hatari kipindi cha pili.

Hata hivyo, Bakari Mwamnyeto, Erasto Nyoni na Shomari Kapombe mabeki wa Stars pamoja na Mohamed Hussein walikuwa na kazi ya kufanya kwa kuwa washambuliaji wa Sudan walikuwa wakiweka ngome lango la Manula.

John Bocco na Msuva walikuwa wakipata tabu mbele kwa kuwa ilikuwa ikiwalazimu kurudi nyuma kuokoa mashambulizi na kutengeneza nafasi za kwenda kufunga, jambo ambalo limewafanya washindwe kufanya hatari kwa Tunisia.Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Novemba 17, Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
 
Taifa Stars ambayo inanolewa na Kocha Etienne Ndayiragije ilikuwa inahitaji ushindi ili kuweka matumaini ya kufuzu kucheza michuano hiyo mikubwa ngazi ya taifa kwa mara ya pili mfululizo baada ya kushiriki ile ya Misri.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news