Polisi, Coastal Union zalazimisha sare, Tanzania Prisons yang'ara

Maafande wa Polisi Tanzania wamelazimishwa sare ya kufungana 1-1 na Coastal Union ya Tanga leo,anaripoti Mwandishi Diramakini.

Mtanange huo umepigwa katika nyasi za Uwanja wa Uhuru uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Bao la kwanza lilitoka kwa Tariq Seif Kiakala wa Polisi Tanzania ndani ya dakika 50 ndipo baada ya dakia ya 75,Raizin Hafidh akaisawazishia timu yake ya Coastal Union.

Kwa matokeo hayo, timu ya Polisi Tanzania inafikisha alama 20 baada ya kucheza mechi 13, ingawa inabaki nafasi ya tano ikizidiwa alama tatu na Ruvu Shooting na Simba SC zinazofuatana nafasi ya tatu na ya nne.

Aidha, kwa matokeo hayo Coastal Union inafikisha alama 16 baada ya mechi 13 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 11 katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Wakati huo huo,Ruvu Shooting kutoka mkoani Pwani imelazimishwa sare ya bila kufungana na Kagera Sugar katika Uwanja wa nyumbani wa Mabatini uliopo mjini Mlandizi mkoani humo.

Kwa matokeo hayo, Ruvu Shooting imefikisha alama 23 baada ya mechi 13 pia na kuendelea kukamata nafasi ya nne, nyuma ya Simba SC yenye alama 23 za mechi 11 hadi sasa.

Awali,Tanzania Prisons iliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Mwadui FC katika Uwanja wa Nelson Mandela uliopo mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.

Lambert Sibiyanka ndani ya dakika ya 23 na Gasper Mwaipasi dakika ya 87 ndio walioiwezesha timu yao kuibuka na alama tatu katika mechi hiyo ya leo.

Aidha, kwa matokeo ya leo, Tanzania Prisons imefikisha alama 19 baada ya mechi 13 na kupanda hadi nafasi ya sita kutoka ya tisa huku Mwadui FC ikiwa na alama 10 baada ya mechi 13 ambapo inakaribia kwenye mkia katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news