Rais Dkt. Mwinyi aanza kazi, Serikali yaitisha wadaiwa sugu

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdalla ameuagiza Uongozi wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) kuwasilishwa ofisini kwake ripoti ya majina ya wadaiwa sugu wote wa madeni ya Serikali ndani ya siku saba ili hatua za kisheria zichukuliwe mara moja dhidi ya wahusika hao, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Amesema wapo baadhi ya wafanyabishara na wawekezaji wenye tabia ya kutumia migongo ya wakubwa kukwepa kulipa kodi kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa jambo ambalo uchangia kudhoofisha ukusanyaji wa mapato yanayohitajika kuendesha Serikali.


Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar, Joseph Abdalla Meza akielezea hatua zinazochukuliwa na bodi hiyo katika kukabiliana na madeni ya wadaiwa sugu wa mapato ya Serikali.

Mheshimiwa Hemed Suleimna Abdalla ametoa agizo hilo alipofanya ziara fupi Novemba 17, 2020 katika makao makuu ya Bodi ya Mapato Zanzibar yaliyopo Mazizini nje kidogo ya jiji la Zanzibar kuangalia utendaji kazi wa taasisi hiyo ya fedha.

Amesema, Bodi ya Mapato Zanzibar ndio tegemeo kubwa la ukusanyaji wa mapato ya Serikali katika kuimarisha uchumi wake. Hivyo bado ipo kazi kubwa ya kuendelea kukusanya kodi hasa kwa wale wajanja wanaodaiwa kodi na hawana dalili wala muelekeo wa kulipa au kupunguza madeni yao.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ametahadharisha kwamba Serikali Kuu haitasita kuwafutia vibali mara moja wawekezaji au wafanyabiashara wote watakaoonyesha dalili ya usugu wa kulipa kodi zao kwa mujibu wa biashara wanazoendesha.

Mapema Meneja wa Madeni wa Bodi ya Mapao Zanzibar, Bi. Asya Abisalami alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba wapo wadaiwa sugu zaidi sita wa hoteli na Wwfanyabiashara wa miradi mikubwa wenye madeni makubwa ya zaidi ya shilingi Bilioni 17 yaliyochukuwa muda mrefu.

Bi.Asya amesema, madeni hayo yamejumuisha pia fedha za baadhi ya wafanyakazi wa hoteli kupitia michango yao ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF) pamoja na leseni za biashara.

Kwa upande wake Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar, Joseph Abdalla Meza amesema, uongozi wa Bodi ya Mapato Zanzibar umekuwa ukichukuwa hatua mbalimbali za kuhakikisha madeni hayo yanaendelea kulipwa na pale muhusika anavyokaidi maamuzi hayo hufikia hatua ya kufutiwa leseni yake ya biashara.

Meza amesema, wapo baadhi ya wadaiwa ambao tayari wamefikishwa kwenye vyombo vya sheria kuhusiana na kukiuka mikataba yao ambapo wengine hujiepusha na adhabu kwa kulipa kadri ya masharti wanayowekewa.

Kamishna huyo wa Bodi ya Mapato Zanzibar amemueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba uongozi wa taasisi hiyo umechukuwa hatua ya kukabiliana na mbinu za baadhi ya washirika wao kwa kufunga vifaa vinavyosaidia kuwatabaini baadhi ya wawekezaji na wafanyabiashara wanaofuta taarifa kwenye mitandao yao.

Amesema, mfumo wa teknolojia unaotumiwa na ZRB hivi sasa unawezesha kutambua hata taarifa zilizofichwa au kufutwa na wateja na hatimae uongozi huchukuwa hatua ya kumuwajibisha muhusika kwa mujibu wa kosa alilofanya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news