Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeendelea kuimarisha usimamizi na udhibiti wa shughuli za gesi asilia katika mkondo wa kati na chini, hatua inayolenga kuhakikisha usalama wa miundombinu, upatikanaji wa huduma bora pamoja na kukuza matumizi ya nishati safi nchini.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, wakati akiwasilisha Hotuba ya Bajeti kwa Mwaka wa fedha 2026/2027 Aprili 22,2026 bungeni Dodoma.
Amesema katika kipindi cha Julai 2025 hadi Machi 2026, EWURA ilifanya kaguzi 68 katika miundombinu ya gesi asilia iliyopo katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani na Dar es Salaam.

Miundombinu hiyo inahusisha mitambo minne ya uchakataji, miwili ya usafirishaji, mtandao wa usambazaji wenye urefu wa kilomita 243 pamoja na vituo 18 vya kujazia gesi asilia iliyoshindiliwa (CNG) kwa magari. Taarifa zinaonesha kuwa miundombinu yote iliyokaguliwa ilikidhi viwango vya ubora vinavyotakiwa.

Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo