Rais Dkt. Mwinyi awapa faraja wafanyabiashara

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussain Ali Mwinyi amefanya ziara katika soko la Kijangwani kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za wafanyabiashara katika eneo hilo, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Katika ziara yake hiyo, Dkt.Hussein amesema ahadi yake ya kuwasaidia wajasiriamali bado ipo pale pale hivyo wasiwe na wasiwasi katika kutatuliwa matatizo yao na sasa yupo mbioni kuwatatulia pamoja na kuwapatia vibali maalum vya kufanyia biashara zao kwa utulivu.


Rais Mwinyi amesema kuwa, anayafahamu matatizo ya wafanyabiashara hao kwani alifika mahali hapo katika kipindi cha kampeni na kusikiliza changamoto zao.

Hata hivyo Rais ameuwagiza uongozi wa Manispaa pamoja na Mkoa kutafuta eneo sahihi la kuwapeleka wafanyabiashara hao na si kuwahamisha katika eneo hilo kwa sasa waachiwe na waendelee na biashara zao katika eneo hilo.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara hao, Mariyam Abdalla amesema kuwa kama wananchi wa kawaida hawawezi kupingana na maamuzi ya serikali ila wanaomba eneo la uhakika ambalo watafanya biashara zao kwa utulivu kwani kitendo cha kuhamishiswa kila siku kinawapotezea mitaji yao.

Akitoa maelezo ya kuhamishwa kwa wafanyabiashara hao Mkuu wa Mkoa wa Mjini, Hassan Khatib Hassan amesema kuondoshwa kwa wafanyabiashara hao ni moja ya mipango ya maendelea ya kujenga Zanzibar mpya na si kuwaonea.

Post a Comment

0 Comments