RC:Kituo cha Kimataifa cha Mabasi Mbezi Luis kinaweza kutumika

Kituo kipya cha mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi cha Mbezi Luis, Dar es Salaam kimeanza rasmi majaribio leo ambapo Mkuu wa Mko, Aboubakar Kunenge amesema kwa sasa kituo hicho kinaweza kuanza kutumika kutokana na miundombinu muhimu ya kituo kuwa katika hali mzuri.

Akizungumza wakati wa zoezi la majaribio lililowahusisha askari wa usalama barabarani na wadau wa vyombo vya usafiri, RC Kunenge ameshuhudia Mabasi yakiingia na kutoka pasipo usumbufu wowote.
 
RC Kunenge amesema kwa sasa kinachoendelea ni matengenezo madogomadogo ya umaliziaji wa jengo na miundombinu mingine ambapo hadi sasa ujenzi umefikia zaidi ya asilimia 90.

Pamoja na hayo RC Kunenge amesema ujenzi wa barabara ya kuingia kituoni hapo nao unaendelea vizuri chini ya Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) ambapo amewahimiza kuongeza kasi.
RC Kunenge ameongeza kuwa, wamejipanga vizuri kuhakikisha maagizo ya Rais Dkt. John Magufuli ya kutaka ujenzi ukamilike mwishoni mwa mwezi huu yanatimia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news