CHADEMA yatoa saa 48 kwa Halima Mdee na wenzake

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa siku mbili kwa wanachama wake 19, ambao jana walikula viapo Bungeni vya kuwa wabunge wa viti maalum bila ridhaa ya chama kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kitakachofanyika Novemba 27, 2020,anaripoti Mwandishi Diramakini.

 

Wabunge hao 19 wa Viti Maalum wakiongozwa na Halima Mdee ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wameapishwa jana katika Viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Spika Job Ndugai.

Wengine ni Asia Mohamed, Felista Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Simon, Anatropia Theonest,Salome Makamba, Conchester Lwamraza, Grace Tendega, Ester Matiko,Secilia Pareso,Ester Bulaya,Agnes Kaiza,Nusrat Hanje,Jesca Kishoa,Hawa Mwaifunga na Tunza Malapo.

Kauli hiyo imetolewa leo Novemba 25, 2002, na Katibu Mkuu wa chama hicho John Mnyika, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa kwa kuwa jambo hilo ni la dharura wameamua kufuata katiba yao inayosema kuwa, hatua zozote zisichukuliwe bila wahusika kuitwa kujieleza ili kujua ni nini kilichowapelekea wao kukisaliti chama.

"Kwa kuwa jambo hili ni la dharura natangaza wito (Public notice), kupitia vyombo vya habari kwa wanachama wetu 19 walioshiriki kwenda kula kiapo jana, kufika makao makuu ya chama bila kukosa siku ya Ijumaaa ya Novemba 27, 2020, saa 2:00 asubuhi, kutoka popote pale walipo kamati kuu inaweza kuchukua hatua za dharura kama itaona maslahi ya jumla ya chama yanaweza kuathiriwa,"amesema Mnyika.

Akizungumzia suala la wabunge hao kula kiapo hicho amesema kuwa, "Mimi kama Katibu Mkuu hakuna fomu yoyote ya mtu yeyote niliyowahi kuijaza popote kuthibitisha uteuzi wa yeyote, hii fomu pia ina sehemu ya kujazwa na kiapo cha hakimu kwahiyo kwa tafsiri nyepesi ni kilichofanyika ni biashara haramu ya kughushi, wameenda kuapishwa bila baraka ya chama,"amebainisha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news