Wabunge Viti Maalum CHADEMA kupewa ushirikiano mkubwa

Spika wa Bunge wa Bunge la Jamhuri bya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Job Ndugai ameahidi kutoa kila aina ya ushirikiano kwa wabunge 19 wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) walioapishwa katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma,anaripoti Mwandishi Diramakini.Novemba 24, 2020 wabunge hao wa Viti Maalum wakiongozwa na Halima Mdee ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wameapishwa.

Wengine ni Asia Mohamed, Felista Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Simon, Anatropia Theonest,Salome Makamba, Conchester Lwamraza, Grace Tendega, Ester Matiko, Secilia Pareso, Ester Bulaya, Agnes Kaiza, Nusrat Hanje, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga na Tunza Malapo.
 
Akizungumza baada ya kuwaapisha wabunge hao, Spika Ndugai ameeleza kuwa atawapa ushirikiano wote ili waweze kutimiza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi.

“Neno langu kwenu nendeni mkawatumikie watanzania, naahidi kuwapa kila aina ya ushirikiano, najua kambi yenu itakuwa ya wabunge wachache wajibu wa spika ni kuwalinda walio wachache, nitajitahidi kuwalinda kuwapa haki ili muweze kutekeleza majukumu yenu ya kuwatumikia Watanzania na muweze kufanya kazi yenu ya kikatiba kwa ukamilifu,”amesema.

Post a Comment

0 Comments