Asanteni! Asanteni! Asanteni! wasomaji, wadau wa Diramakini

Uongozi wa Kampuni ya Diramakini Business Limited ambao ni wamiliki wa mtandao wa www.diramakini.co.tz na huduma nyingine unapenda kuchukua nafasi hii kukutakia heri ya Mwaka Mpya wa 2021, mpendwa msomaji wetu na wadau wetu katika habari ambao wamekuwa wakishirikiana nasi tangu tulipoanza kutoa huduma zetu kupitia maudhui ya mtandaoni.

Umekuwa sehemu kubwa ya mafanikio yetu kuanzia mwezi Agosti 2020, tulipopata leseni rasmi, tunahaidi kufanya maboresho zaidi ya namna bora ya kuwahabarisha kadri Mwenyenzi Mungu atakavyotujalia nguvu na uwezo wa kubuni mambo mapya zaidi. 

Pale palipokuwa na mapungufu tunaomba msamaha, kwa kuwa tunaamini mwaka uliopita ulikuwa wa kujifunza njia bora ya kuwaletea habari. 

Kipekee tunachukua nafasi hii kuwapongeza sana wadau wetu ambao wamekuwa mstari wa mbele kutupa michango mbalimbali kwa ajli ya kuwawezesha usafiri na mawasiliano wawakilishi wetu waliopo ndani na nje ya Tanzania. 

Tumeona namna ambavyo michango yenu imekuwa nuru na faraja kwetu, tunawaomba msisitie kuendelea kutuunga mkono kwa kiasi chochote kile ili tuweze kuyafikia maeneo mengi zaidi katika kuibua, kuandaa na kuwapasha habari motomoto za uhakika na kwa wakati. 

Ukiguswa kutuchangia au kutupa habari, maoni usisite kuwasiliana nasi kupitia barua pepe ya diramakini@gmail.com au +2557 19254464.  

Mtandao wetu wa www.diramakini.co.tz utaendelea kuwapasha habari kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza kila siku kwa saa 24, asante na kwa mara nyingine tena, uongozi na wafanyakazi wa Diramakini Business Limited unawatakia heri ya mwaka mpya wenye mafanikio tele.

Post a Comment

0 Comments