Harmonize afungua ukurasa mpya kwa Diamond Platinum 2021

Msanii, mwandishi wa nyimbo, mwimbaji na Mkurugenzi wa Konde Music Worldwide, Rajabu Abdul Kahali (Harmonize) ambaye amezaliwa Machi 15,1990 amekiri wazi kuwa bila mkono wa Diamond Platnumz, mafanikio yake ya sasa si kitu, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Kutokana na hatua hiyo, Harmonize amemuomba kaka yake huyo Nasibu Abdul Juma Issack (Diamond Platnumz) ambaye amezaliwa Oktoba 20, 1989 apokee salamu zake za heri ya mwaka mpya 2021. 

Pia Harmonize amemuomba Diamond Platinum kukaa na kutafakari kwa kina kuhusu uamuzi wake wa kuondoka katika lebo yake ya WCB. 

Amesema, kutokana na mchango wa CEO huyo wa WCB ameweza kuwa kinara ndani na nje, hivyo mafanikio hayo ni ishara njema kwa yeye kumshika mkono. 

Diamond Platnumz ambaye ni msanii wa Kimataifa na Mtanzania kupitia nyimbo za bongo flava, mwimbaji, mchezaji, mzee wa tuzo na mfanyabiashara kupitia shughuli mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari vya Wasafi TV na Wasafi FM, siku za karibuni waliingia katika mgogoro na Harmonize kutokana na sababu ambazo wanazijua wenyewe.

Post a Comment

0 Comments