Watanzania watakiwa kudumisha mambo makuu matatu

Watanzania wametakiwa kujenga tabia ya kudumisha Upendo,Amani na Mshikamano kuanzia ngazi ya familia ili kuweza kujenga taifa imara litakalokuwa na viongozi imara na wenye upendo kwa watu wake, anaripoti Danson Kaijage (Dodoma).

Wito huo umetolewa na Mchungaji Emmanuel Nhonya wakati wa ibada maalumu ukoo wa Ligoha,Nhonya na Mboga masali iliyofanyika nyumbani kwa Jackson Ligoha kata ya Dodoma Makulu jijini hapa.

Mchungaji Nhonya amesema kuwa watanzania kwa sasa wanaanza kupoteza utamaduni wao wa kale wa kupendana na kujaliana na kuanza kufuta utaratibu wa nchi za Magharibi.

Katika ibada hiyo iliyokuwa na malengo ya kukutanisha koo hizo kwa lengo la kujengeana misingi ya upendo na kutambuna kwa kumshirikisha Mungu, mchungaji huyo amesema kwa sasa familia nyingi zimepoteza upendo.

"Kama jamii hususani familia moja moja pamoja na koo mbalimbali zikipoteza upendo moja kwa moja tutakosa watu ambao ni wazalendo katika familia zao.

"Ili kuwa na taifa lenye viongozi waadilifu ni lazima wajengwe kwenye misingi ya Upendo,umoja na mshikamano,na ili vitu hivyo vipatikane inatakiwa kuanzia katika familia na ukoo kwa ujumla.

"Kwa sasa upendo,umoja na ushirikiano umepotea katika familia nyinyi imefikia hatua hata watoto wa ndugu na ndugu hawafahamiani jambo ambalo ni hatari kwa afya ya familia husika,ukoo na taifa kwa ujumla," amesema Mchungaji Nhonya.

Kwa upande wake Jackson Ligoha amesema ibada za kifamilia na kiukoo ni kati ya Ibada muhimu ambazo zinajenga udugu,umoja,upendo na ushirikiano huku zaidi wakiwa wanajengwa katika misingi ya Kimungu.

Amesema iwapo jamii itakuwa na hofu ya kimungu ni rahisi zaidi kupata viongozi ambao watakuwa na hofu ya Kimungu na kwa kufanya hivyo viongozi katika sekta mbalimbali hawawezi kuwa mafisadi wala walarushwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news