Waziri Mkuu apokea nyumba 14 vya madarasa kutoka TPB Plc

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amepokea vyumba 11 vya madarasa, ofisi mbili za walimu, samani na chumba maalumu cha wasichana vilivyojengwa na Benki ya TPB PLC katika shule ya msingi Nandagala wilayani Ruangwa, Lindi kwa gharama ya shilingi milioni 164.902, anaripoti Mwandishi Maalum Diramakini.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kupokea vyumba 11 vya madarasa vilivyojengwa na kukarabatiwa na Benki ya Posta Tanzania katika Shule ya Msingi ya Nandagala wilayani Ruangwa kwa gaharama ya shilingi milioni 164, Desemba 28, 2020. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Sabasaba Moshingi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Amepokea mradi huo wa ujenzi na ukarabati wa vyumba vya madarasa leo Desemba 28, 2020 alipotembelea shule hiyo akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani Ruangwa. Waziri Mkuu ameupongeza uongozi wa benki hiyo. 

Waziri Mkuu amewataka wazazi, walimu na wanafunzi wahakikishe majengo hayo yanatunzwa ili yaweze kutumika kwa muda mrefu. “Tunataka majengo haya kama yalivyo leo yaendelee kuwa hivihivi. Tuyatunze haya majengo, Wanafunzi msifanye majaribio ya kuandika ukutani wala kupiga chapa ya miguu kwenye ukuta. Tunawashukuru TBP kwa kutukabidhi madarasa haya ambayo manne ni mapya na saba yamekarabatiwa.” 

Akizungumzia kuhusu ufaulu, Waziri Mkuu amesema kati ya wanafunzi 63 waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu katika shule hiyo 57 wamefaulu na sita tu ndio hawakufaulu. Ameagiza watoto wote waliofaulu wapelekwe shule na wale sita waliosalia watapelekwa chuo cha VETA kinachotarajiwa kufungulia mwaka 2021 wilayani Ruangwa.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama dawati baada ya kupokea vyumba 11 vya madarasa vilivyojengwa na kukarabtiwa na Benki ya Posta Tanzania katika Shule ya Msingi ya Nandagala wilayani Ruangwa kwa gaharama ya shilingi milioni 164, Desemba 28, 2020. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama dawati baada ya kupokea vyumba 11 vya madarasa vilivyojengwa na kukarabtiwa na Benki ya Posta Tanzania katika Shule ya Msingi ya Nandagala wilayani Ruangwa kwa gaharama ya shilingi milioni 164, Desemba 28, 2020. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa TPB Bank PLC, Sabasaba Moshingi alisema utekelezaji wa mradi huo ni muendelezo wa mpango wa benki hiyo wa kurejesha sehemu ya faida wanayoipata kwa jamii kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa miundombinu ya elimu na afya. 

Amesema mradi huo ulihusisha ukarabati wa vyumba saba vya madarasa pamoja na ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa vinne, ofisi mbili za walimu, stoo, ukarabati wa matundu 28 ya vyoo, ujenzi wa chumba maalumu cha wasichana pamoja na utengenezaji wa samani za walimu ikiwa ni pamoja na meza 13 na viti 13. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi (wa tatu kulia) wakifungua vyumba 11 vya madarasa vilivyojengwa na kakarabatiwa na Benki ya Posta Tanzania katika Shule ya Msingi ya Nandagala wilayani Ruangwa kwa gaharama ya shilingi milioni 164, Desemba 28, 2020. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Benki ya Posta baada ya kupokea vyumba 11 vya madarasa vilivyojengwa na kukarabatiwa na benki hiyo katika Shule ya Msingi ya Nandagala wilayani Ruangwa kwa gaharama ya shilingi milioni 164, Desemba 28, 2020. Kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Sabasaba Moshingi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Naye Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa mradi huo Hamza Mkuyanda alisema kukamilika kwake kumeleta manufaa mengi yakiwemo mazingira bora ya kuvutia katika ufundishaji na ujifunzaji kwa walimu na wanafunzi na hivyo kuongeza kiwango cha taaluma shuleni hapo. 

Pia, Waziri Mkuu alipokea vyumba vitatu vya madarasa na chumba kimoja cha walimu vilivyojengwa na wadau wa elimu katika shule ya msingi Mkata iliyoko kijiji cha Namahema wilayani Ruangwa kwa thamani ya shilingi milioni 76.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news