Juma Ngamia kuchuana na Murtaza Mangungu uwenyekiti Smba SC

Kamati ya uchaguzi ya Simba SC imempitisha aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa na Mbunge wa zamani wa jimbo la Chemba, Juma Nkamia kugombea uenyekiti wa klabu hiyo, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Katika uchaguzi huo mdogo uliopangwa kufanyika Februari 7, mwaka huu, Nkamia aliyewahi kuwa Katibu Mwenezi wa Simba SC awali, atapambana na Mbunge wa zamani wa Kilwa, Murtaza Mangungu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Simba SC, Boniface Lihamwike amesema, wawili hao ndio watakaopambana katika uchaguzi huo mdogo kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mwenyekiti, Swedi Nkwabi Septemba 14, mwaka 2019.

Hatua hiyo inakuja baada ya kuenguliwa kwa Mbunge wa Jimbo la Mlalo wilayani Lushoto mkoani Tanga, Rashid Abdallah Shangazi na Bittony Innocent Mkwakisu na Khamis Omar Mtika. 

Aidha, Mjumbe wa Bodi ya Wakurungenzi ya Simba, Mwina Kaduguda aliteuliwa kuwa Kaimu Mwenyekiti wa klabu hiyo baada Mkwabi kujiuzulu.

Post a Comment

0 Comments