Leicester City yang'ara Ligi Kuu England, Paris St-Germain nao Ufaransa

Klabu ya Leicester City imekwea mpaka nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu nchini England baada ya kuiadhibu Southampton goli 2-0 mchezo uliopigwa dimba la King Power, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Kiungo mshambuliaji wa England James Maddison aliitanguliza mbele Leicester City katika dakika ya 37 kabla ya Harvey Barnes ajaongeza bao la pili kwa timu hiyo inayonolewa na kocha wa zamani wa Liverpool, Brendan Rodgers.

Ushindi kwa City unaifanya kukwea mpaka nafasi ya pili alama moja dhidi ya vinara Manchester United ambao watakuwa na mtanange dhidi ya mabingwa watetezi Liverpool, wakati huo huo Southampton wanabakia nafasi ya nane alama tatu nje ya nne bora.

Mbali na hayo, Paris St-Germain wamerudi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Ufaransa Ligue 1 baada ya kupata ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya Angers.
Picha na Reuters.

Mlinzi wa pembeni wa matajiri hao wa Jiji la Paris, Layvin Kurzawa aliipa uongozi kwa goli pekee katika mchezo huo ambapo sasa kocha Mauricio Pochettino na kikosi chake wanafikisha mechi saba bila kupoteza.

Pochettino hakuwa sehemu ya kikosi hicho uwanjani baada ya siku moja kabla ya mchezo kubainika kuwa na dalili za maambukizi ya Covid-19 hivyo alitakiwa kujitenga mwenyewe.

PSG wanapanda mpaka nafasi ya kwanza pointi mbili wazi dhidi ya timu iliyopo nafasi ya pili Lyon ambao wanamchezo mkononi kwa sasa.

Post a Comment

0 Comments