Mama Diamond aonyesha picha ya Baba halisi wa Diamond Platinum na Ricardomomo


Kwa mara ya kwanza Mama Mzazi wa Diamond ameonesha sura ya Baba Mzazi wa Msanii Diamond. 

Na hiyo ni baada ya muda mfupi kutoka kuthibitisha Baba halisi wa Msanii huyo ambaye pia ni Baba Mzazi wa Ricardomomo.

Wakati huo huo, Ricardomomo amesema kuwa, "Mimi na Diamond ni wa Baba mmoja,"amesema huku mama yao akirejea kuwa, Mama Diamond (Dangote) amethibitisha kuwa, Mzee Abdul sio baba yake na Daimond bali ni Baba Mlezi.

Akiongea na Wasafi Fm, Ricardomomo amethibitisha kuwa mwaka 1999 aliletewa Diamond na marehemu Baba yake yeye akiwa uwanjani na kuambiwa ni mdogo wake ingawa watu wengi hawajui.

Mbali na hilo Mama Dangote amepigiwa simu na kueleza kuwa Diamond na Ricardo Momo ni ndugu na wamechangia Baba Mzazi mzazi na kueleza kuwa Mzee Abdul sio Baba yake mzazi na Diamond bali ni baba yake mlezi, bali baba yake anaitwa Salum Idd Nyange.

Post a Comment

0 Comments