Mkuu wa Mkoa mstaafu Brigedia Jenerali Emmanuel Maganga afariki

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu, Emmanuel Maganga amefariki dunia usiku wa Januari 21,2021, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa, Brigedia Jenerali mstaafu Maganga amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Jeshi mkoani Tabora.

Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga alistaafu mwezi Julai, mwaka 2020 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alimteua, Bw. Thobias Andengenye ambaye aliwahi kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuwa Mkuu wa mkoa wa Kigoma kuchukua nafasi yake. 
 
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dkt.Philemon Sengati, Mheshimiwa Maganga amefariki Dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Milambo mkoani Tabora usiku huu.

Post a Comment

0 Comments