Serikali yatoa mwezi mmoja Kituo cha Afya Vikindu kifunguliwe

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dkt. Festo John Dugange ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani kufungua Kituo cha Afya Vikindu ifikapo Januari 30, 2021 ili wananchi waweze kupata huduma za afya msingi zilizokusudiwa ikiwa ni pamoja na huduma za kliniki za mama na mtoto na matibabu kwa wagonjwa wa nje, anaripoti Mwandishi Diramakini (Pwani).
Dkt.Dugange ametoa maagizo hayo wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo baada ya kubaini kuwa mradi uliojengwa kwa fedha za Serikali ya shilingi 200 umekamilika miezi sita iliyopita bila kutoa huduma kwa wananchi kwa maelezo kuwa wanasubiri vifaa toka Bohari ya Dawa nchini. 

Aidha, Dkt. Duganhe ameitaka Menejimenti ya Mkuranga kujiongeza kwa kununua vifaa vya msingi vya kuanzia ili kukata kiu waliyonayo wananchi ya kuonja matunda ya mafanikio ya Serikali yao inayoongozwa na Dkt.John Pombe Joseph Magufuli.

Awali wakati wa ziara hiyo, Naibu Waziri Dkt. Festo John Dugange alifanya kikao cha ndani na viongozi wa wilaya, kisha kukagua hali ya utoaji huduma katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya Mkuranga, ujenzi wa barabara ya Vikindu-Sangatini unaogharimu shilingi milioni 400 na kusimamiwa na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) na kisha kuhitimisha kwa kukagua ujenzi wa stendi ya kisasa ya mabasi Kipala-mpakani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news