Utabiri wa hali ya hewa/ Weather Forecast today January 22nd, 2021

 

Utabiri wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo kuanzia 3:00 usiku wa leo tarehe 22-01-2021 unaletwa na mchambuzi Tunza Sanane kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Weather forecast for the next 24 hours starting 21:00 tonight on today January 22nd, 2021 as presented by analyst Thereza Ngassa from Tanzania Meteorological Authority (TMA).

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO: TAREHE: 22/01/2021

Mikoa ya Songwe, Mbeya, Rukwa, Iringa, Njombe, Ruvuma na Kusini mwa mkoa wa Morogoro: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

.........

Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu,Tabora, Dodoma  Singida na Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

.........

Mikoa ya Lindi na Mtwara: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.

........

Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia),

Tanga pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba, Kilimanjaro, Manyara na Arusha: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

.......

ANGALIZO:

VIPINDI VYA UPEPO MKALI UNAOFIKIA KM 40 KWA SAA VINATARAJIWA KATIKA MAENEO YA MWAMBAO WA

ZIWA NYASA.

.........

VIWANGO VYA JOTO, VYA JUA KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:

MJI               Kiwango cha juu     Kiwango cha chini 

                     cha  joto                 cha joto

ARUSHA       29°C                       15°C

D'SALAAM   32°C                        24°C

DODOMA     26°C                       18°C

KIGOMA       29°C                       21°C

MBEYA         26°C                      17°C

IRINGA         25°C                      17°C

NJOMBE      20°C                       13°C

MWANZA    28°C                       19°C

TABORA       29°C                       18°C

TANGA         31°C                       22°C

ZANZIBAR    32°C                       25°C

..........

Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 30 kwa saa kwa Pwani yote; kutoka Kaskazini Mashariki

kwa Pwani ya Kaskazini, na kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.

Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Makubwa kiasi.

Matarajio kwa siku ya Jumapili tarehe 24/01/2021: Kupungua kwa mvua katika maeneo ya nyanda za juu Kusini

magharibi na Pwani ya Kusini.

Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 22/01/2021.

Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.


MATARAJIO YA HALI MBAYA YA HEWA

JUMAMOSI: 23/01/2021

ANGALIZO la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mwambao wa Ziwa Nyasa.

UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI

KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI

.........

Athari zinazoweza kujitokeza:

Pamoja na ucheleweshwaji wa baadhi ya shughuli za uvuvi.

.........

Tafadhali zingatia na ujiandae.

........

JUMAPILI: 24/01/2021

ANGALIZO la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mwambao wa Ziwa Nyasa.

.........

UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI

KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI

........

Athari zinazoweza kujitokeza

Pamoja na ucheleweshwaji wa baadhi ya shughuli za uvuvi.

.........

Tafadhali zingatia na ujiandae.

Post a Comment

0 Comments