Utabiri wa hali ya hewa/ Weather Forecast today January 24th, 2021


Utabiri wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo kuanzia 3:00 usiku wa leo tarehe 24-01-2021 unaletwa na mchambuzi Akili Mwangaza kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Weather forecast for the next 24 hours starting 21:00 tonight on today January 24th, 2021 as presented by analyst Akili Mwangaza from Tanzania Meteorological Authority (TMA).

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO: TAREHE: 24/01/2021.

………………..........

Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Songwe, Mbeya, Rukwa, Iringa, Njombe, Kigoma, Tabora, Katavi na Ruvuma: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

.........

Mikoa ya Morogoro, Lindi, Mtwara, Dodoma, Singida, Kilimanjaro, Manyara, Arusha, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Tanga pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

.......

VIWANGO VYA JOTO KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:

MJI               Kiwango cha juu     Kiwango cha chini 

                     cha  joto                 cha joto

ARUSHA       28°C                       16°C

D'SALAAM   32°C                        25°C

DODOMA     28°C                       20°C

KIGOMA       29°C                       21°C

MBEYA         27°C                      16°C

IRINGA         28°C                      17°C

NJOMBE      21°C                       13°C

MWANZA    29°C                       19°C

TABORA       29°C                       19°C

TANGA         31°C                       22°C

ZANZIBAR    32°C                       26°C

..........

Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 20 kwa saa kwa Pwani yote; kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.

Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi madogo.

Matarajio kwa siku ya Jumanne tarehe 26/01/2021: mabadiliko kidogo

Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 24/01/2021.

Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

Post a Comment

0 Comments