Utabiri wa hali ya hewa/ Weather Forecast today January 25th, 2021

  Utabiri wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo kuanzia saa 3:00 usiku wa leo tarehe 25-01-2021 unawasilishwa na Doreen Mwara kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

 
UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO:
TAREHE: 25/01/2021
 
Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Songwe, Mbeya, Rukwa, Iringa, Njombe, Kigoma, Tabora, Katavi, na Ruvuma Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
..........
Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Visiwa vya Unguja na Pemba, Dodoma, Singida, Morogoro, Lindi na Mtwara Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi, katika maeneo machache na vipindi vya jua.
.............
Mikoa ya Kilimanjaro, Manyara na Arusha Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
............
VIWANGO VYA JOTO VYA JUA KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:
MJI Kiwango cha juu Kiwango cha chini
cha joto cha joto
ARUSHA 29°C 16°C
D'SALAAM 32°C 25°C
DODOMA 29°C 19°C
KIGOMA 29°C 21°C
MBEYA 24°C 15°C
IRINGA 27°C 16°C
NJOMBE 21°C 12°C
MWANZA 27°C 19°C
TABORA 29°C 19°C
TANGA 31°C 24°C
ZANZIBAR 33°C 26°C
...........
Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 20 kwa saa kwa Pwani yote; kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.
Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Madogo.
Matarajio kwa siku ya Jumatano tarehe 27/01/2021:
Mabadiliko kidogo.
Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 25/01/2021.
Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.
............

Post a Comment

0 Comments