Watoto milioni 140 kuzaliwa mwaka huu wa 2021

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limekadiria kuwa mwazoni mwa mwezi huu wa Januari 2021 zaidi ya watoto 371,5004 watazaliwa duniani kote,anaripoti Mwandishi Diramakini.
Picha na UNICEF.

UNICEF kupitia taarifa yake wanataraji kwamba,zaidi ya nusu ya watoto wa Mwaka Mpya watazaliwa katika nchi 10 ikiwemo India (takriban 59,995),China (35,615), Nigeria (21,439), Pakistan (1 4,164), Indonesia (12,336), Ethiopia (10,2006), Marekani (10,312), Misri (9455), Bangladesh (9,236) na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC (8,640). 

Kupitia uchambuzi wa sensa ya kitaifa na data ya usajili na pia ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Mtazamo wa Idadi ya Watu, UNICEF inakadiria kuwa jumla ya takriban watoto milioni 140 watazaliwa duniani mwaka huu wa 2021, wakiwa na wastani wa umri wa kuishi wa miaka 84. 

Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Ariana Fowler anasema,watoto waliozaliwa Siku ya Mwaka Mpya wamekuja kwenye Ulimwengu tofauti kabisa na mwaka mmoja uliopita.

Kwa mustakabali wa watoto hao, ametaka jamii ya kimataifa kufanya kazi pamoja akisema, "ufanye mwaka 2021 uwe aina ya Mwaka wa haki zaidi, salama na afya kwa watoto,"amesema wakati ambao mwaka 2021 ni kumbukumbu ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa UNICEF. 

Katika kipindi cha mwaka mzima, UNICEF itafanya shughuli kadhaa za kumbukumbu na wadau wake, wakati ikiendelea kulinda watoto kutoka kwenye mizozo, magonjwa na kutengwa na pia kuhakikisha inawatetea. 

Fowler ameongeza kuwa, wakati Ulimwengu unakabiliwa na janga jipya la virusi vya Corona (COVID-19), kushuka kwa uchumi, kuongezeka kwa umaskini na kuongezeka kwa ukosefu wa usawa, kazi ya UNICEF ni muhimu zaidi kuliko hapo awali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news