Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP-CENTRE) na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya kimkakati inayolenga kurahisisha ushiriki wa wafanyabiashara kwenye miradi mikubwa ya kimaendeleo.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa PPP-CENTRE, David Kafulila, alisema ushirikiano huo unalenga kutafsiri maono ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan ya kuipa sekta binafsi nafasi kubwa zaidi katika kukuza uchumi.
Kafulila afafanua kuwa jukumu kuu la kituo hicho ni kuhakikisha muundo wa miradi inayofanywa kwa ubia inawanufaisha watu wote; Mwekezaji, kampuni binafsi, Serikali na jamii nzima.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo






















