Waziri Mkuu ashiriki maziko ya dada wa Spika Ndugai

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameshiriki maziko ya dada wa Spika wa Bunge, Job Ndugai, Mary Ndugai aliyefariki dunia Januari 23, 2021 wilayani Mpwapwa, Dodoma, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa pole kwa familia ya Dada wa Spika wa Bunge la Tanzania, Marehemu Mary Yustino Ndugai, kwenye makaburi ya Ving’awe katika Wilaya Mpwapwa mkoani Dodoma, Januari 25, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).Maziko hayo ya Mary Ndugai yamefanyika leo Januari 25, 2021 katika makaburi ya Ving’awe wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa ibada ya mazishi ya Dada wa Spika wa Bunge la Tanzania, Marehemu Mary Yustino Ndugai, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Dayosisi ya Mpwapwa, Dodoma. Januari 25, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Akizungumza baada ibada ya kumuombea marehemu Mary iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania jimbo la Mpwapwa, Waziri Mkuu amewaomba wafiwa wawe na subira na utulivu katika kipindi hiki kigumu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiweka shada la maua katika kaburi Marehemu Mary Yustino Ndugai, ambaye ni Dada wa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai kwenye makaburi ya Ving’awe katika Wilaya Mpwapwa mkoani Dodoma, Januari 25, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima wakati wa ibada ya mazishi ya Dada wa Spika wa Bunge la Tanzania, Marehemu Mary Yustino Ndugai, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Dayosisi ya Mpwapwa, Dodoma. Januari 25, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, akitoa heshima wakati wa ibada ya mazishi ya Dada yake, Marehemu Mary Yustino Ndugai, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Dayosisi ya Mpwapwa, Dodoma. Januari 25, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

“Nimekuja kuungana nanyi kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan kutoa pole kwa Mheshimiwa Spika Job Ndugai kufuatia msiba mzito wa kuondokewa na dada yake mpendwa Mary,”amesema.

Waziri Mkuu amesema msiba huo ni mzito na jukumu kubwa ni kumuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu pahala pema, hivyo amewaomba watoto wa marehemu, ndugu na jamaa wawe watulivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai na mkewe akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu dada yake, Mary Yustino Ndugai kwenye makaburi ya Ving’awe katika Wilaya Mpwapwa mkoani Dodoma, Januari 25, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Kwa upande wake, Spika wa Bunge, Job Ndugai amewashukuru viongozi wa dini, Serikali na waombolezaji kwa kujitokeza na kuifariji familia kufuatia msiba huo. Pia amewashukuru Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya wilaya ya Mpwapwa ambapo marehemu alikuwa akitibiwa.

Viongozi wengine waliohudhuria maziko hayo ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Mwigulu Nchemba, Katibu wa Bunge Stephen Kigaigai na baadhi ya wabunge.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news