Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kifo cha Maalim Seif, atangaza siku tatu za maombolezo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli alimtumia salamu za rambirambi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi kufuatia kifo cha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kilichotokea leo Februari 17, 2021 wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Katika salamu hizo, Rais Magufuli amemuomba Rais Mwinyi kufikisha salamu za pole kwa familia ya marehemu, Wazanzibari wote, wanachama wa ACT-Wazalendo, ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na kifo hicho.

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. Natoa pole kwa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Dkt. Mwinyi, familia, Wazanzibari, wanachama wa ACT-Wazalendo na Watanzania wote. Mungu amuweke mahali pema peponi, Amina,”amesema Rais Magufuli.

Pia amewataka wafiwa wote kuwa na moyo subira, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki cha majonzi na amemuombea marehemu apumzike mahali pema.

Kufuatia msiba huo,Rais Magufuli ametangaza siku tatu za maombolezo ya Kitaifa kuanzia jana Februari 17, 2021 ambapo bendera zote zitapepea nusu mlingoti.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Magufuli


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news