Rais Magufuli azindua viwanda mkoani Morogoro



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifungua Kiwanda cha kusafisha na kufungasha mazao cha Mahashree Tanzania Limited kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kufungua Kiwanda cha Kuchakata Mpunga cha MW Rice Millers limited kilichopo Kihonda mkoani Morogoro leo tarehe 12 Februari 2021. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia moja ya bidhaa za mchele wa aina mbalimbali katika Kiwanda cha MW Rice Millers limited mara baada ya kukifungua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia na kuwashukuru wananchi wa mkoa wa Morogoro mara baada ya kufungua Kiwanda cha MW Rice Millers limited kilichopo Kihonda mkoani Morogoro. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare, Mkurugenzi wa Kiwanda cha Ngozi cha Taifa-Morogoro Rostam Aziz wakati akifungua Kiwanda hicho cha Ngozi cha Taifa-Morogoro kilichopo Kihonda katika Manispaa ya Morogoro leo tarehe 12 Februari 2021. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kufungua Kiwanda cha Ngozi cha Taifa kilichopo Kihonda katika Manispaa ya Morogoro leo tarehe 12 Februari 2021.
Moja ya hatua za uchakataji wa Ngozi katika Kiwanda cha Ngozi cha Taifa kilichopo Kihonda mkoani Morogoro. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia moja ya hatua za uchakataji wa Ngozi katika Kiwanda cha Ngozi cha Taifa mara baada ya kukifungua. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi mara baada ya kufungua Kiwanda cha Ngozi cha Taifa-Morogoro kilichopo Kihonda mkoani Morogoro. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Ngozi ambayo imeshatengenezwa katika Kiwanda hicho cha Taifa kilichopo Morogoro. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi mara baada ya kufungua Kiwanda cha kusafisha na kufungasha mazao cha Mahashree Tanzania Limited kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro. Sehemu ya Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kufungua Kiwanda cha kusafisha na kufungasha mazao cha Mahashree Tanzania Limited kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro. (Picha zote na IKULU).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news