Magazeti leo Machi 20,2026

Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. Suzan S. Kaganda, amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Shirika la Kikanda la Haki Miliki Afrika (African Regional Intellectual Property Organization-ARIPO) lenye ofisi zake mjini Harare, Zimbambwe.
Wawakilishi hao ni Mkuu wa Kitengo cha Hakimiliki na Haki Shirikishi, Bi. Maureen Fondo pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Utafutaji na Uchunguzi, Bw. Said Ramadhan, ambao wote ni raia wa Tanzania wanaofanyakazi katika taasisi hiyo ya kikanda.

Wawakilishi hao walifika Ubalozini kwa lengo la kujitambulisha kwa Mheshimiwa Balozi Kaganda pamoja na kulitambulisha shirika hilo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku na kuimarisha ushirikiano wa kikazi.

Katika mazungumzo hayo, Mhe. Balozi Kaganda aliwapongeza kwa mchango wao katika shirika hilo, akisisitiza kuwa uwepo wao unasaidia kuitangaza Tanzania kimataifa pamoja na kuhakikisha maslahi ya nchi yanalindwa na kupewa kipaumbele katika taasisi na mashirika ya kimataifa yanayoshughulikia masuala ya haki miliki na ubunifu.
Aidha, wawakilishi hao waliishukuru Ofisi ya Ubalozi kwa ushirikiano mzuri, wakieleza kuwa shirika hilo lilianzishwa kufuatia makubaliano yaliyofikiwa mwaka 1976 katika mji wa Lusaka, kupitia Makubaliano ya Lusaka ya tarehe 9 Desemba 1976.

Waliongeza kuwa taasisi hiyo inalenga kusimamia na kuratibu masuala ya haki miliki na ubunifu kwa nchi 22 wanachama, ikiwemo Tanzania, kwa lengo la kuhamasisha ubunifu, kulinda haki za wabunifu na kuchochea maendeleo ya kiuchumi barani Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here