Magazeti leo Machi 23,2026

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Felchesmi Mramba ametangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika sekta ya nishati nchini, akizialika kampuni na wawekezaji wa kimataifa kuchangamkia nafasi hizo ili kuchochea ukuaji wa sekta hiyo.
Akizungumza katika kikao maalum cha India–Africa Partnership kilichofanyika wakati wa mkutano wa Bharat Electricity 2026 unaoendelea nchini India, Mhandisi Mramba amesema Tanzania ina mazingira rafiki ya uwekezaji na inaendelea kujipambanua kama moja ya maeneo yenye fursa kubwa katika sekta ya nishati barani Afrika.

Ameeleza kuwa fursa hizo zinapatikana katika maeneo mbalimbali ikiwemo miradi ya kuzalisha umeme, kusafirisha na kusambaza umeme, pamoja na uwekezaji katika nishati jadidifu kama jua, upepo, jotoardhi na umeme wa maji. Aidha, ametaja pia uwekezaji katika nishati safi ya kupikia kuwa ni eneo muhimu linalopewa kipaumbele na Serikali.

Mhandisi Mramba ameeleza kuwa Tanzania inaendelea kukuza sekta ya umeme ili kukidhi ongezeko la mahitaji linalochochewa na ukuaji wa viwanda na ongezeko la matumizi ya umeme mijini na vijijini, akibainisha kuwa uwezo wa uzalishaji umefikia takribani megawati 4,500 na unatarajiwa kufikia megawati 8,000 ifikapo mwaka 2030.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here