TAKUKURU yaokoa madai ya mishahara ya walimu, wafanyakazi Misungwi English Medium

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Misungi Mkoa wa Mwanza imeendelea kutekeleza majukumu yake ambapo leo imerejesha fedha ilizookoa kwa wahusika,a naripoti Mwandishi Diramakini.

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Bi.Emma Mwasyonge amesema, wamerejesha fedha hizo kiasi cha sh.milioni 6,543,500 ambazo ni sehemu ya fedha za mishahara ambayo ni madeni ya walimu na wafanyakazi wa Shule ya Misungwi English Medium.

Amesema, fedha hizo walikuwa wanaidai kampuni ya Tanzania Education Supporting Agency (TESA) iliyokuwa nimeingia mkataba na shule hiyo.

Pichani ni Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Bi.Emma Mwasyonge akikabidhi fedha hizo sh.milioni 6,543,500 kwa Mkurugenzi wa Shule ya Misungwi English Medium, Bw. Ephraim Ngoso leo Februari 10, 2021.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news