🔴𝐋𝐈𝐕𝐄: Maelfu ya wananchi wanauaga mwili wa Hayati Dkt.Magufuli leo Machi 24,2021 jijini Mwanza/ Farewell the fallen hero of Africa 🌍


MATANGAZO MUBASHARA TAZAMA JUU
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mwili wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Machi 24, 2021.
Mwili wa hayati Dkt. John Pombe Magufuli, ukiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza, Machi 24, 2021.    Msafara wa Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ukipita katika barabara ya Airport kuelekea katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kwa ajili ya shughuli za kuagwa na maelfu ya Wananchi wa mkoa wa Mwanza na mikoa jirani leo tarehe 24 Machi 2021.
Msafara wa Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ukiwasili katika uwanja wa CCM Kirumba kwa ajili ya shughuli za kuagwa na maelfu ya Wananchi wa mkoa wa Mwanza na mikoa jirani leo tarehe 24 Machi 2021.
Makamanda wa JWTZ wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. (Picha na Ikulu).

Post a Comment

0 Comments