Polisi Dar waua majambazi watano, 10 mbaroni wizi wa pikipiki 16

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwaua majambazi watano na kukamata silaha moja bastola aina ya STAR iliyofutwa namba ikiwa na risasi tatu ndani na maganda mawili ya risasi, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Dar es Salaam).

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Dar es Salaam SACP Lazaro Mambosasa ameyasema hayo leo Machi 1, 2021 wakatika akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam.

"Mnamo Februari 27, 2021 majira ya saa kumi na mbili asubuhi huko maeneo ya Kivule kwa Iranga, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kupitia kikosi chake cha kupambana na ujambazi lilifanikiwa kuwaua majambazi watano waliokuwa kwenye gari namba T 836 DHF aina ya Toyota Noah.

"Majambazi hao wapatao sita wakiwa kwenye gari hiyo kwenda kufanya uhalifu maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, lakini kabla hawajatimiza lengo lao, kikosi kazi cha Jeshi la Polisi kiliweka mtego na kufanikiwa kuzuia ujambazi huo kwa kutaka kuwakamata wahalifu hao, lakini majambazi hao walitoka kwenye gari na kuanza kukimbia huku wakiwarushia askari risasi na hatimaye askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwapiga risasi majambazi watano ambao walifariki dunia papo hapo na jambazi mmoja kufanikiwa kukimbia huku akifyatua risasi hovyo na kumjeruhi askari mmoja,"amesema Kamanda Mambosasa.

Ameongeza kuwa, baada ya kuwapekua majambazi hao walikutwa na bastola moja ikiwa na risasi tatu ndani ya magazine na maganda mawili ya bastola na iili ya marehemu imeifadhiwa Hospitali yaTaifa Muhimbili.

WATUHUMIWA KUMI MBARONI KWA WIZI WA PIKIPIKI NA KUPATIKANA PIKIPIKI 16

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuanzia Februari Mosi hadi Februari 28, mwaka huu lilifanya oparesheni maalum ya kuwasaka wezi wa pikipiki na kufanikiwa kuwakamata wakiwa na pikipiki 16 zinazodhaniwa kuwa za wizi.

Kwa mujibu wa Kamanda Mambosasa, watuhumiwa hao ni;
1.Stephen Paul (38),Mkazi wa Ulongoni A
2.Salum Mustafa (28),Mkazi wa Kigogo
3.Nsajigwa Kaisi (25), Mkazi wa Mongo la Ndege A na watuhumiwa wengine saba.
Oparesheni hiyo ilifanyika baada ya kupokea taarifa toka kwa wahanga wa matukio hayo ambayo yalikithiri katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.

Aidha watuhumiwa hao wamekuwa wakiiba pikipiki katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na kuzipeleka kwa Madalali ili kuziuza sehemu mbalimbali.
watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na pikipiki zifuatazo;
(i)MC 967CRT aina ya Boxer (ii) MC 922CSL aina ya Boxer
((iii))MC 646 CMS aina ya Boxer(iv)MC 900 CRC aina ya Boxer
(v)MC 218 CSP aina ya Boxer(vi)MC 339 CRQ aina ya Boxer
(vii)MC 677CNQ aina ya Boxer(viii)MC 804 CRU aina ya Boxer
(ix) MC 271 CPT aina ya Boxer (x) MC 618 CRC aina ya Boxer
(xi) MC 885 CKB aina ya Boxer (xii) MC 832 CQF aina ya TVS (xiii) MC 634 CKA aina ya TVS (xiv) MC 412 CKP aina ya TVS (xv) MC 543 AWN aina ya Boxer (xvi) MC 735 CMF aina ya Boxer.

Jeshi la Polisi kanda Maalum Dar es salaam linaendelea na oparesheni na misako dhidi ya wizi wa pikipiki, magari na wahalifu wa makosa mengine.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news