Rahimi avuruga dili la Namungo FC, Raja na Pyramids zang'ara Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika

Nyota wa Raja Club Athletic, Soufiane Rahimi ndani ya dakika 54 amezima ndoto za Namungo FC kujipatia alama tatu ugenini baada ya kuzitikisa nyavu zao, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI.

Penalti ya Rahimi imewawezesha kuzoa alama zote tatu katika mtanagne huo wa Machi 10, 2021 katika Kundi D michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Ni baada ya kuchapwa 1-0 na wenyeji hao katika dimba la Mohamed V lililopo mjini Casablanca nchini Morocco.

Chini ya kocha Hemed, Namungo FC katika mtanange huo uliochezeshwa na refa Hassen Corneh wa Liberia aliyekuwa anasaidiwa na Boris Ditsoga na Felix Abaa Eyaga wote wa Gabon alimtoa kwa kadi nyekundu beki wa Ramadhani Haruna Shamte kufuatia kumuonyesha kadi mbili za njano dakika ya 22 na 66, hivyo kuifanya Namungo kucheza pungufu.

Aidha, kutokana na matokeo hayo, Namungo FC ipo nafasi ya tatu kwenye kundi hilo huku Nkana ikiwa mkiani kufuatia wenyeji wengine, Pyramids kuwapa kichapo kikali Nkana FC ya Zambia 3-0.

Ni kupitia mabao ya Mahmoud Wadi dakika ya pili, Islam Issa dakika ya tisa na Mohamed Farouk dakika ya 90 katika dimba la 30 June Stadium, Cairo nchini Misri.

Katika mtanange huo ambao ulisimamiwa na refa Georges Gatogato, nyota wa Nkana FC, Stephen Chulu alipigwa kadi ya njano.

Hata hivyo, mechi zijazo, Namungo FC watakuwa wenyeji wa Pyramids katika dimba la Azam Complex lililopo Kata ya Chamanzi, Manispaa ya Temeke, Dar es Samaa Machi 17, mwaka huu ambapo Nkana FC watawaalika Raja Casablanca katika dimba la Levy Mwanawasa Ndola nchini Zambia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news