Ligi Kuu Tanzania Bara yazidi kuwa mwiba, Simba yagawana alama na Tanzania Prisons

Simba SC wamelazimishwa sare ya 1-1 na timu ya Tanzania Prisons ndani ya dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Dar es Salaam).

Luis Jose Miquissne ndiye aliyeiokoa Simba baada ya kuisawazishia bao dakika ya tano ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika tisini katika mtanange huo wa Machi 10, 2021. 

Prisons Tanzania walitangulia kwa bao la Salum Kimenya dakika ya 55 baada ya mshambuliaji wa Simba SC kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kope Mutshimba Mugalu kukosa penalti.

Licha ya kucheza pungufu, baada ya Jumanne Elfadhil Nimkiza kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 43, Tanzania Prisons walionyesha juhudi ambazo zimewasaidia kugawana alama moja moja.

Chini ya kocha raia Mfaransa Didier Gomes Da Rosa , Simba SC inafikisha alama 46 baada ya kucheza mechi 20 na kuendelea kushika nafasi ya pili nyuma ya watani wao wa jadi, Yanga SC wenye alama 50 baada ya kucheza mechi ishirini na tatu.

Post a Comment

0 Comments