🔴𝐋𝐈𝐕𝐄:Rais Samia anapokea ripoti ya CAG na TAKUKURU Ikulu ya Chamwino leo


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akielekea katika ukumbi wa Mikutano wa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma kwa ajili ya kupokea Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG kwa mwaka wa Fedha 2019/2020 leo tarehe 28 Machi 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 28 Machi, 2021 amepokea taarifa za mwaka za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI.

Hafla ya kupokea taarifa hizo imefanyika Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai, Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Mawaziri, Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Makatibu Wakuu na viongozi wakuu wa taasisi na idara za Serikali. 

LIVE TAZAMA HAPA CHINI

Mhe. Rais Samia ameipongeza ofisi ya CAG na TAKUKURU kwa kazi za ukaguzi na uchunguzi zilizofanywa katika mwaka 2019/20. Ameiagiza ofisi ya CAG kuongeza wataalamu wa ukaguzi ili waweze kukagua mashirika mengi zaidi na miradi mingi zaidi hususani iliyopo mikoani ambayo maendeleo yake hayaridhishi.

Kutokana na taarifa ya CAG kuonesha kuwa kuna kusuasua kwa utekelezaji wa mapendekezo juu ya usimamizi wa hesabu za Serikali na hali isiyoridhisha ya mashirika na taasisi za Serikali, Mhe. Rais Samia ameahidi kuongeza msukumo katika utekelezaji wa mapendekezo hayo na kuchukua hatua za haraka dhidi ya mashirika na taasisi ambazo zimetajwa kufanya vibaya kutokana na wizi na upotevu wa fedha za umma.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere akionesha moja ya Taarifa zake za ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/20 kabla ya kuziwasilisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo tarehe 28 Machi 2021 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere wakati akitolea maelezo moja ya Taarifa zake za ukaguzi leo tarehe 28 Machi 2021 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo wakati akitolea Maelezo moja ya Taarifa yake ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa mwaka 2019/20
Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga mara baada ya kutoka katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu ya Chamwino. (Picha zote na Ikulu).

Ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko kufuatia taarifa za kuwepo upotevu wa fedha kiasi cha shilingi Bilioni 3.6 na ameiagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi katika mamlaka hiyo.

Mhe. Rais Samia amemuagiza CAG Charles Kichere kufanya ukaguzi wa fedha zote zilizotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kati ya mwezi Januari na Machi, 2021.

Ameitaka Ofisi ya CAG na TAKUKURU kushirikiana kuweka sawa mifumo ya fedha inayotumiwa na hazina ili kuondokana na changamoto na athari za kuwepo mifumo mingi tena isiyowasiliana na ambayo inasababisha upotevu mkubwa wa fedha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Salvatory Mabeyo na viongozi wengine baada ya hafla ya kupokea ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na TAKUKURU Ikulu Chamwino
jijini Dodoma leo Jumapili Machi 28, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe Samia Suluhu Hassan baada ya hafla ya kupokea ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na TAKUKURU Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo Jumapili Machi 28, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe Samia Suluhu Hassan akiagana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama baada ya hafla ya kupokea ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na TAKUKURU Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo Jumapili Machi
28, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe Samia Suluhu Hassan akiagana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt Bashiru Ally pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama baada ya hafla ya kupokea ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na TAKUKURU Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo Jumapili Machi 28, 2021.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro baada ya hafla ya kupokea ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na TAKUKURU iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo Jumapili Machi 28, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali Bw. Charles Kichere baada ya hafla ya kupokea ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na TAKUKURU iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo Jumapili Machi 28, 2021


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya kupokea ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na TAKUKURU iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo Jumapili Machi 28, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt Bashiru Ally, Katibu Mkuu Ikulu Dkt Moses Kusiluka na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (Utumishi) Dkt.Laurean Ndumbaro baada ya hafla ya kupokea ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na TAKUKURU iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo Jumapili Machi 28, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiaga ili kuondoka eneo la tukio baada ya hafla ya kupokea ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na TAKUKURU iliyofanyika katika
Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo Jumapili Machi 28, 2021.


Kuhusu mashirika yasiyofanya vizuri amemtaka CAG kutomung’unya maneno akisema “mashirika yasiyofanya vizuri, naomba sana CAG ulimi wako usiwe na utata, kama kuna shirika halifanyi vizuri tuambie hili halifanyi vizuri, kama bodi haisimami vizuri tuambie bodi hii haisimami vizuri, kwa sababu tutakaposema mapungufu ndipo tutakapoweza kurekebisha na kufanya vizuri zaidi, tukinyamaziana na kuficha sura hatutarekebisha na tutawaumiza wananchi, naomba sana ripoti yako iwe wazi zaidi, utakaponiletea ukaguzi wa mashirika naomba uwe wazi zaidi ili tujue tunachukua hatua gani”.

Kwa upande wa TAKUKURU, Mhe. Rais Samia ameitaka taasisi hiyo kuongeza juhudi zaidi kwa kuharakisha kufikisha Mahakamani kesi za rushwa na ufisadi, kuachana na kesi ambazo hazina msingi wa kushinda na ameitaka taasisi hiyo kujielekeza zaidi katika masuala yanayohusiana na rushwa na yale yanayopaswa kufanywa na vyombo vingine viachiwe vyombo husika.

Amehimiza uadilifu kwa watumishi wa TAKUKURU ambao wamekuwa wakiwafichua mashahidi na watoa taarifa na pia ametaka taasisi hiyo ipanue uwigo wa kufuatilia vitendo vya rushwa ikiwemo uvujaji wa mitihani, kuboresha mifumo yake ya kukabiliana na rushwa na ufisadi na ishirikiane na taasisi nyingine katika kufanikisha vita dhidi ya rushwa.

Mhe. Rais Samia amewahakikishia Watanzania kuwa atasimama imara kulinda makusanyo na matumizi ya fedha za Serikali pamoja na vita dhidi ya rushwa.

Katika taarifa yake CAG Charles Kichere amesema katika mwaka 2019/20 ofisi yake imetoa jumla ya hati 900 za ukaguzi (zikiwemo 243 za Serikali Kuu, 185 Serikali za Mitaa, 165 za Mashirika ya Umma, 290 za miradi na 17 vyama vya siasa) ambapo 800 (89%) zinaridhisha, 81 zina mashaka (9%), 10 mbaya (1%) na hati 9 alishindwa kutoa maoni.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brig. Jen. John Mbungo amesema katika mwaka 2019/20 taasisi hiyo ilifanikiwa kutekeleza majukumu yake kwa asilimia 89.8 ikilinganishwa na mwaka uliopita ilipotekeleza majukumu yake kwa asilimia 88.1 ongezeko ambalo limetokana na kukamilisha uchunguzi kwa majalada 1,079 ikilinganishwa na majalada 911 ya mwaka uliopita.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news