Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheruka amewaomba wadau na wananchi wa mkoa Kagera kuendelea kuichangia timu ya Nyaishozi FC ambao ni mabingwa wa ligi Mkoa Kagera wanaoenda kushiriki ligi ya mabigwa wa Mikoa (RCL2021) ambapo timu hiyo imepagwa kundi D na itachezea mechi katika kituo cha Katavi,anaripoti Eliud Rwechungura (Karagwe).
Mheruka ameyasema leo,Machi 1, 2021 alipokuwa akipokea jezi za wachezaji na pesa ya kuisaidia timu kutoka kwa Kampuni ya Hlucky Kombucha Investment ambao ni wazalishaji wa kinywaji cha Kombucha Ginger Drink ambao ni wadhamini wa timu ya Nyaishozi FC.
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheruka (kulia) akipokea jezi kutoka Mkurugenzi wa Kampuni Hlucky Kombucha Investment, Bw. Hamis Jumanne ambao ni wadhamini wa timu ya Nyaishozi FC mabingwa wa ligi mkoa Kagera wanaoenda kushiriki ligi ya mabigwa wa Mikoa (RCL2021) ambapo timu hiyo itachezea mechi katika kituo cha Katavi imepagwa kundi D, nyuma ni kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Karagwe Kagera, Leo, Machi 01, 2021.Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni Hlucky Kombucha investment, Bw. Hamis Jumanne amesema kuwa Kampuni yake imeamua kuunga mkono timu ya Nyaishozi FC ili kuunga mkono michezo ndani ya mkoa lakini pia kuumunga mkono Rais wetu pia Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa ambaye ndie Mbunge wa Jimbo la Karagwe kwa sababu tuna timu ambayo imewakilisha wilaya Karagwe vizuri na sasa inaendelea kuuwakilisha Mkoa vizuri katika ligi ya Mikoa (RCL2021).
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheruka (kulia) akipokea kiasi cha pesa kutoka Mkurugenzi wa Kampuni Hlucky Kombucha Investment, Bw. Hamis Jumanne ambao ni wadhamini wa timu ya Nyaishozi FC mabingwa wa ligi mkoa Kagera wanaoenda kushiriki ligi ya mabigwa wa Mikoa (RCL2021) ambapo timu hiyo itachezea mechi katika kituo cha Katavi imepagwa kundi D, nyuma ni kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Karagwe Kagera leo, Machi 1, 2021.
Mkurugenzi wa Kampuni Hlucky Kombucha Investment, Bw. Hamis Jumanne akiwa katika picha pamoja na Katibu Msaidizi wa msaidizi wa Chama cha mpira mkoa Kagera, Majaliwa Said na Kocha Msaidizi wa timu ya Nyaishozi Fc, Jonson Majara mara baada ya kukabidhi jezi ya pesa za kusaidia timu ya Nyaishozi FC mabingwa wa ligi mkoa Kagera wanaoenda kushiriki ligi ya mabigwa wa Mikoa (RCL2021) ambapo timu hiyo itachezea mechi katika kituo cha Katavi imepagwa kundi D, Karagwe Kagera leo, Machi 01, 2021.Awali, Katibu Msaidizi wa msaidizi wa Chama cha mpira mkoa Kagera, Majaliwa Said amewashukuru wananchi na wadau wote wanaoendelea kujitoa na kuunga mkono timu ya Nyaishozi maana timu bado ni changa kushiriki ligi hizi na amehaidi atashirikiana na timu kuhakikisha inapata ushindi katika ligi hiyo inayoanza Machi 04, 2021 huko mkoani Katavi.