Utabiri wa hali ya hewa/ Weather Forecast today Mach 5th, 2021

 
UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO: TAREHE: 05/03/2021.

Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Mbeya, Songwe, Iringa, Rukwa, Njombe, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Kigoma, Tabora, Katavi, Kusini mwa Mkoa wa Morogoro, Dodoma na Singida inatarajiwa Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

.........

Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Kilimanjaro, Manyara na Arusha, Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro inatarajiwa Hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

........

Visiwa vya Unguja na Pemba, Mkoa wa Tanga kunatarajiwa Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.

........

KIWANGO CHA JUU CHA JOTO KINATARAJIWA KUWA NYUZI JOTO 34 (34°C) KATIKA VISIWA VYA ZANZIBAR

Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 30 kwa saa; kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.

Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Makubwa kiasi.

Matarajio kwa siku ya Jumapili tarehe 07/03/2021: Mabadiliko kidogo.

Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 05/03/2021.

Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news