Vikao vya Kamati za Bunge kuanza Machi 8 hadi 26, 2021 jijini Dodoma



Kamati za Kudumu za Bunge zitaanza kukutana siku ya Jumatatu tarehe 8 hadi 26 Machi, 2021 Jijini Dodoma kwaajili ya vikao vinavyotangulia kabla ya Mkutano waTatu wa Bunge uliopangwa kuanza tarehe 30 Machi, 2021.

Kwa ratiba hiyo, Waheshimiwa Wabunge wote wanatakiwa kuwasili Jijini Dodoma Jumapili tarehe 7 Machi, 2021 kwaajili ya vikao hivyo.

Shughuli za Kamati katika kipindi hicho zitakuwa ni: -

i) Kupokea mapendekezo ya Serikali kuhusu Mpango, kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 kwa mujibu wa Kanuni ya 116(1) ya Kanuni za Kudumuza Bunge Toleo la Juni, 2020. Wabunge wote watahusika na shughuli hii;

ii) Kutembelea na Kukagua Utekelezaji wa Miradi iliyotengewa fedha kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ili kuzingatia masharti ya Kanuni ya 117(1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Juni, 2020. Wajumbe wa Kamati za Kisekta watahusika na shughuli hii;

iii) Ziara za Ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za Umma kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa, Serikali Kuu na Taasisi za Umma ili kuzingatia masharti ya sehemu ya Nne ya Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Juni, 2020;

iv) Uchambuzi wa taarifa za Uwekezaji uliofanywa na Serikali kupitia mashirika, taasisi na Kampuni ambazo Serikalii na Hisa pamoja na ziara ya kukagua shughuli za uwekezaji zilizofanywa na Serikali kupitia Mashirika, Taasisi na Kampuni ambazo Serikali ina Hisa. Wajumbe wa Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma watahusika na shughuli hii;

v) Uchambuzi wa Taarifa za Utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2020/2021 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kwa mujibu wa Kanuni ya 117(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Januari, 2020. Wajumbe wa Kamati za Kisekta, Kamati ya Bajeti na Kamati ya Masuala ya Ukimwi watahusika na shughuli hii;

vi) Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Pili wa Bunge ili kutekeleza masharti ya kifungu cha 11 cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Juni, 2020;

vii) Mashauriano kati ya Kamati ya Uongozi na Kamati ya Bajeti kuhusu masuala muhimu yatakayokuwa yamejitokeza kwenye Kamati za Kisekta wakati wa uchambuzi wa Taarifa za utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/20 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2020/21. Shughuli hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 117(5) na 117(6) ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Juni, 2020.

Ratiba ya Shughuli za Kamati za Bunge inapatikana katika Tovuti ya Bunge ambayo ni www.parliament.go.tz

Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa,

Ofisi ya Bunge,

DODOMA.

04 Machi, 2021.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news