Dkt.Hassan Abbasi: Serikali ipo tayari kufanyia kazi hoja na maoni yenu

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi amesema Serikali ipo tayari kufanyia kazi hoja, Maoni na mapendekezo kuhusu sera na sheria kwenye sekta ya habari kwa ajili ya kuboresha utendaji Kazi wa sekta hiyo,anaripoti Mwandishi Wetu (MAELEZO).

Akizungumza katika mdahalo wa majadiliano kuhusu kutafuta njia inayohusisha viashiria vya Habari katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa, Dkt. Abbasi amewataka wadau wa sekta hiyo, kupeleka maoni na hoja Serikalini kuhusu sera na sheria ili kuboresha sekta hiyo.

“Serikali ipo tayari kuifanyia kazi hoja yoyote hasa pale ambapo patahusu sera na sheria ili kuwawezesha waandishi wa habari kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi” amesema Dkt. Abbasi.

Aidha, amesema Serikali imejitahidi kuwapa nafasi wanawake kuongoza katika vyombo vya Habari na kutolea mfano wa Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN) na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Dkt. Abbasi aliwashukuru wadau wa mashirika yaliyoandaa mdahalo huo na kuwaomba UNESCO na wadau wengine kuendelea na utamaduni huo Ili kujenga sekta ya Habari kuwa na weledi.

“UNESCO na Wadau wengine waandae midahalo hiyo angalau mara mbili kwa mwaka na Serikali itashirikiana nao Ili kukuza uelewa katika sekta ya Habari”. Dkt.Abbasi.

Kwa upande wao washiriki wamesema wakati Serikali inafanya marekebisho ya sheria, wakumbuke kuhusu suala la Usawa wa jinsia kwenye vyombo vya Habari, ili kurahisha waandishi wa Habari Wanawake kufanya kazi kwa amani, hoja ambayo Katibu Mkuu aliijibu kwa kusema “penye mambo ya kijinsia ni vizuri yakazungumzwa, ni muda mwafaka wa kuyawasilisha”

 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news