Makachero wa Tanzania wakamata tani moja ya madawa ya kulevya aina ya Heroin huko Kilwa Masoko

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kushirikiana na Kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Wananchi (JWTZ) leo Aprili 24, 2021 wamekamata zaidi ya tani moja ya madawa ya kulevya aina ya Heroin, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI.
Baadhi ya watuhumiwa katika tukio hilo la madawa ya kulevya.
Jahazi linalohusishwa kusafirisha dawa za kulevya.
Sehemu ya dawa za kulevya.

Dawa hizo zimekamatwa eneo la Kilwa Masoko katika Bahari ya Hindi zikisafirishwa kwa kutumia Jahazi la Al Arbo, likiwa na watuhumiwa saba ndani yake.

Waliokamatwa ni Jan Mohammad Miranira aliyekuwa nahodha wa jahazi hilo na wenzake sita ambapo jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi bado zinaendelea kwani simu yake inaita bila kupokelewa.

Katika tukio hilo, watu saba wamekamatwa ambao ni kama ifuatavyo;

Waliokamatwa ambao wote si raia wa Tanzania ni nahodha wa jahazi hilo, Jan Mohammad Miranira, Amir Hussein, Yusuph Bin Hamad, Salim Bin Mohammad, Ikbal Pakir Mohammad, Jawid Nuhan Nur Mohammad na Mustaphar Nowani Kadirbaksh..

Kamishna wa DCEA, Gerald Kusaya amesema raia hao wamekamatwa usiku wa kuamkia leo Jumamosi Aprili 24, 2021 eneo la Kilwa Masoko wakisafirisha dawa hizo.

Amebainisha kuwa watu hao bado wapo safarini kuletwa nchi kavu na watakapofika watahojiwa kuhusu dawa hizo, walikuwa wanakwenda wapi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news