Mbunge Mtenga apendekeza namna mpya ya kumuenzi Hayati Magufuli, agusia ajira, kilimo

Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini, Hassan Sulemani Mtenga ameishauri Serikali kumuenzi aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Magufuli kwa kumjengea alama ya kumbukumbu kwa kuweka bango kubwa katika makutano ya barabara mkoani Morogoro ikiwa ni hatua ya kumuenzi kwa vitendo, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI.
Akizungumza wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2021/2022 bungeni jijini Dodoma, Mtenga amesema kama ilivyo kwa viongozi wengine ni vyema hayati Magufuli kufanyiwa hivyo.

“Nimekuwa mtumishi wa CCM kwa muda mrefu na nimepitia nafasi mbalimbali mpaka hapa nilipofikia hapa niliposimama ninaweza kuzungumza, lakini sitamsahau mheshimiwa Hayati Dkt.John Pombe Magufuli ,nimekuwa mzungumzaji sana, lakini sio tu Magufuli ila kwa viongozi waliotangulia mbele ya haki.

“Nakumbuka wakati Sokoine amefariki, lakini kwa kipindi chote takribani miaka 10 ilikuwa inaonesha tumkumbuke lakini tulikuwa tunasikia kwa asasi mbalimbali jinsi ya kuenzi viongozi wetu.

“Rai yangu nataka nishauri Rais Magufuli amekuwa ni rais bora barani Afrika na ni kiongozi ambaye marais wa Afika walikuwa wanataka kuinga mfano sasa mheshimiwa Naibu Spika ikipendeza pale Morogoro Round about pale tukaweke picha yake kama ni legancy ambayo ameiacha Magufuli na sisi tufike kuwaonesha watanzania kuwa tunamuunga mkono kwa vitendo,”amesema Mtega.

Katika hatua nyingine Mtega amempongeza Naibu Waziri wa Kilimo, Husein Bashe kwa kuweza kuwasaidia katika uuzaji wa zao la korosho.

“Lakini mimi nataka kumpongeza Bashe tulivyokuja Disemba kuapa nilimweleza kuhusu zao la korosho na TMX kule Mtwara nakushukuru sana umekuwa msikivu na umetuelewa watu wa Mtwara.

“Ni vyema wabunge wengine wakamjua TMX ,kule kwangu Mtwara zao kubwa la biashara ni korosho tunapopeleka dalali kwa mkulima na vyombo ambavyo vipo leo kwa mfano TMX nilikuwa nasoma kwenye ripoti yao wanasema watakuja kuwa madadali, lakini udalali wao korosho zao zitanunuliwa online.

“Kwahiyo makampuni yote mnayoyaona yaliyoko Tanzania hususani Mtwara makampuni haya yanawazawa na matajiri wengine wako Vietnam ,India na maeneo mengine tukizungumzia TMX wao wamekuwa wakala namba moja tunazungumzia mfanyabiasha aliyoko Mtwara tayari ameshapoteza ajira kwa sababu korosho zitanunuliwa online na mfanyabishara aliyeko India.

“Na kampuni iko na wafanyakazi kama 20 watapunguzwa atabaki mmoja kwa hiyo mimi niipongeze serikali kwa kuwa wasikivu na kukubaliana kuwa TMX ifike mahali ikae pembeni,”ameeleza.

Pamoja na hayo Mtega ameitaka serikali kuangalia jinsi ya kuwawezesha vijana kujiajiri katika kilimo.

“Tumekuwa tukizungumza ajira kwa vijana hili ni janga lakini sisi wabunge wa Mtwara tuna maeneo mengi ya mapori yanahitaji kufanyiwa maandalizi kwa kilimo, lakini kwa jinsi tulivyoandaa vijana wetu hawawezi kushindana kwenda shambani kulima bila serikali kuwekeza.

“Nataka nitoe mfano leo serikali inatoa matibabu kwa vijana walioathirika na dawa za kulevya tunawatibu kwa gharama kubwa, lakini kuna asilimia 10 ambayo serikali inasema ni ya vijana ,wanawake na walemavu wanatakiwa kuzipata.

“Tuende sasa na mpango endelevu ambao vijana wataenda shambani serikali iwawezeshe vijana hawa wakalime kilimo cha kisasa ili tutoe ajira mpya tofauti na zamani,”ameshauri Mtega.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news