Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devotha Mdachi asimamishwa kazi

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro leo amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devotha Mdachi kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha.
Waziri Ndumbaro ametoa maamuzi hayo leo mkoani Dar es Salaam ambapo amesema uchunguzi huo hauhusiani na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

"Nafasi ya Mdachi itakaimiwa na Betrita James ambaye ni Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi TANAPA, hatuwezi kumchunguza mtu akiwa kakalia kiti hichohicho,"amesema Waziri huyo.

Pia Dkt. Damas Ndumbaro ameielekeza Bodi ya Wakurugenzi ya TTB kuwasimamisha kazi watumishi wengine wanaohusika na tuhuma hizo kwa kuwa suala hilo lipo chini ya  Mamlaka yao ili waweza kupisha uchunguzi dhidi ya madai yanayowakabili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news