Nyalandu ang'atuka CHADEMA arejea CCM tena

“Ninampongeza rais kwa uongozi wako shupavu. Nakushukuru kwa kukubali kunipokea na kunisamehe pamoja na kuniruhusu kurejea chamani, hakuna furaha izidiyo furaha ya mtoto arejeapo nyumbani. Wimbo wa bwana hauimbiki katika nchi ya ugenini, Mzee Sumaye (Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye), Lowassa (Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa) na Dkt. Slaa (aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Chadema,Wilbroad Slaa) ni mashahidi wa hilo;... anaripoti Mwandishi Diramakini (Dodoma).
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kati, Lazaro Nyalandu leo Aprili 30, 2021 baada ya kutangaza kurejea CCM.

Nyalandu amechukua uamuzi huo baada ya kukihama chama hicho miaka kadhaa iliyopita.

Mheshimiwa Nyalandu ametangaza uamuzi wake huo mbele ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan katika mkutano mkuu maalum wa chama hicho tawala uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Nyalandu ambaye ni Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii katika Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete alijitoa CCM Oktoba 30, 2017 na baadaye alijiunga CHADEMA ambako alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama kanda hiyo.

Post a Comment

0 Comments