RAIS DKT.MWINYI AFANYA ZIARA JENGO LA ABIRIA LA TERMINAL III

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, ujenzi wa jengo jipya la abiria (Terminal III) katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume unapaswa kwenda sambamba na utoaji wa huduma bora kwa wasafiri, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Zanzibar).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali baada ya kumaliza ziara yake kutembelea jengo jipya la Abiria la Terminal 3 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.(Picha na Ikulu).

Dkt.Mwinyi amesema hayo leo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, wakati alipolitembelea Jengo jipya la Abiria (Terminal III) lililo katika hatua za mwisho kukamilika ujenzi wake.

Amesema, ujenzi wa jengo hilo umefanywa ili kuimarisha upatikanaji wa huduma bora kwa wasafiri, hivyo akawataka wasimamizi wa ujenzi kuhakikisha kasoro mbalimbali zilizopo katika jengo hilo zinarekebishwa ili kuwepo utoaji mzuri wa huduma.

Rais Dkt.Mwinyi alisema kuwa, ameridhishwa na hatua iliyofikiwa ya ujenzi huo na kuwataka wasimamizi wa ujenzi kurekebisha mapungufu madogo madogo ili kuwa na uwanja wa kisasa na kuepuka hali iliyopo katika jengo la zamani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitembelea jengo jipya la Abiria la Terminal 3 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Kitwana Mustafa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi.Mhandisi Zena Ahmed Said.(Picha na Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitembelea jengo jepya la Abiria la Terminal 3 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar,akimsikiliza Msimamizi wa Ujenzi wa Serikali wa jengo hilo Mhandisi Yassir De Coster wakati wa ziara yake leo 14—4-2021.(Picha na Ikulu).Aliyataja maeneo yanayohitaji kushughulikiwa kuwa ni pamoja na kuongeza vizimba vya Uhamiaji, eneo la ukaguzi wa mizigo pamoja na kuongeza mashine kwa watendaji wa masuala ya‘Custom’.

Dkt. Mwinyi aliwataka wasimamizi wa ujenzi huo kuhakikisha kunakuwepo mabango yanayoainisha taarifa za safari za ndege,kama ilivyo katika viwanja vyote vya Kimataifa Duniani, jambo ambalo halijafanyika hadi hivi sasa.

Aidha, aliwataka kukamilisha hatua mbali mbali zilizobaki mbele ya jengo hilo, ikiwemo upandaji wa majani, ujenzi wa uzio na barabara ili kuupa haiba Uwanja huo, akibainishaku wa sura ya nchi huanzia pale mtu anaposhuka.

Nae Katibu Mkuu Wizara Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Amour Hamil Bakar,alisema ujenzi wa jengo hilo uko hatua za mwisho kukamilika, ambapo unatarajiwa kukabidhiwa Serikalini mapema mwezi wa Mei, 2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akitembelea Jengo jipya la Abiria la Terminal 3 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kuangalia maendeleo ya ujenzi huo leo 14-4-2021, na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe.Rahma Kassim Ali na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Ndg.Amour Hamil Bakari, wakati wa ziara yake kutembelea ujenzi wa jengo jipya la Abiria la Terminal 3 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Mhe. Rahma Kassim Ali na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Kitwana Mustafa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Dkt.Juma Malik.(Picha na Ikulu).

Alisema, ujenzi huo umefikia zaidi ya asilimia tisini, na kusema baadhi ya mambo yatakayoshughulikiwa katika kipindi kifupi kijacho kuwa ni pamoja na ushughulikiaji wa mifumo ya‘Internet’, mifumo ya Uhamiaji pamoja na mifumo ya ukaguzi.

Karika ziara hiyo, Rais Dk. Mwinyi alitembelea maeneo mbali mbali ya jengo hilo, ikiwemo eneo la ukaguzi wa mizigo, eneo la Usalama , ukaguzi wa Paspoti, eneo la Abiria wanaosubiri ndege, vyumba vya wageni mashuhuri (VIP), eneo la wasafiri wa nje, eneo la kupokelea mizigo, eneo la wasafiri wa nje na ndani pamoja na sehemu ya Abiria wanaosubiri ndege.

Aidha, katika ziara hiyo Dkt. Mwinyi aliambatana na viongozi mbalimbali wa Serikali, akiwemo Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Rahma Kassim Ali, Katibu wa Baraza Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa, pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news