Rais Samia atoa pole ajali iliyoua watu 10, kujeruhi wilayani Same



Watu 10 wamefariki dunia huku wengine wakijeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea Kijiji cha Kirinjiko wilayani Same Mkoa wa Kilimanjaro, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI.

Aidha, baadhi ya waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea jioni ya Aprili 13, mwaka huu baada ya gari aina ya Toyota Alphard kugongana uso kwa uso na gari jingine aina ya Toyota Hiace ni waombolezaji waliokuwa wakitoka mkoani Arusha kwenda Lushoto mkoani Tanga.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Amon Kakwale amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo. Hata hivyo, kutokana na ajali hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa ndugu , jamaa na marafiki waliondokewa na ndugu zao huku akiwaombea majeruhi wapone haraka.

"Nawaombea marehemu wapumzike mahali pema peponi na majeruhi wapone haraka. Aidha, nawasihi watumiaji wa barabara kuzingatia sheria za barabarani ili kuepusha ajali,"ameeleza Rais Samia kupitia ukuta wake wa mtandao wa kijamii.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news