UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO APRILI 26,2021

Utabiri wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo kuanzia saa 3:00 usiku wa leo 26/04/2021 umeletwa na mchambuzi Thereza Ngasa.

Mikoa ya Mwanza, Kagera, Geita, Mara, Simiyu, Shinyanga, Kigoma, Tabora, Katavi,Lindi, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Mikoa ya Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, Tanga na Morogoro, Lindi , Mtwara, Kilimanjaro, Arusha na Manyara: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

............................

Mikoa ya Rukwa, Mbeya, Njombe, Songwe, Iringa na Ruvuma: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.

..............................

Mikoa ya Singida na Dodoma: inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi kwa maeneo machache na vipindi vya jua.

................................

KIWANGO CHA JUU CHA JOTO NI NYUZI JOTO 30 ( 30°C ) KATIKA MIJI YA TANGA, DAR ES SALAAM NA TABORA.

............................

Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 30 kwa saa Kutoka Kusini Mashariki kwa Pwani yote.

Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Makubwa kiasi.

Matarajio kwa siku ya Jumatano tarehe 28/04/2021: Mabadiliko kidogo.

Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 26/04/2021.

Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news