AFUNGWA JELA MIAKA 30 KWA KUPATIKANA NA DAWA ZA KULEVYA

Na Diramakini (diramakini@gmail.com)

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kumfunga jela miaka 30 mtu aitwaye MPESO NJANGAJE MWAMPONZA [49] Mkazi wa Ikukwa kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya aina ya Bhangi kiasi cha Debe 03 nyumbani kwake.
Mtuhumiwa alifikishwa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya tarehe 19.05.2021 kwa kuhutuma za kupatikana na bhangi na alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.

Aidha mtuhumiwa anaendelea na kesi nyingine ya mauaji kwani mnamo tarehe 24.05.2020 majira ya saa 05:00 alfajiri huko Kitongoji cha Kiwanja, Kijiji na Kata ya Ikukwa, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya, mtuhumiwa MPESO NJANGAJE MWAMPONZA [49] Mkazi wa Ikukwa anatuhumiwa kutenda kosa la mauaji ya ELIAS MIYOMBE [40].

KUPATIKANA NA POMBE MOSHI [GONGO].

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia WAKATI EDSON [53] Fundi Ujenzi, na Mkazi wa Kiwira na wenzake 09 kwa tuhuma za kupatikana na Pombe Haramu ya Moshi [Gongo] ujazo wa lita 15.

Watuhumiwa kwa pamoja walikamatwa katika msako uliofanyika huko maeneo ya Vilabu vya Pombe Kiwira vilivyopo Kata ya Kiwira, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa akiwa na wenzake wakinywa na kuuza pombe hiyo haramu wakiwa wameijaza kwenye chupa ndogo 43.

KUPATIKANA NA MALI YA WIZI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Polisi nchini Malawi na Polisi wa Kimataifa limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa SAMWEL MWANG’OMBE [46] Mkazi wa Uyole kwa tuhuma za kupatikana na mali ya wizi Bajaji yenye namba za usajili MC.321 CSA aina ya TVS.

Mtuhumiwa alikamatwa jijini Mbeya na katika mahojiano alikiri kuiba Bajaji hiyo tarehe 18.12.2020 huko Uyole na kisha kuipeleka nchini Malawi kuiuza. Baada ya taarifa hizo kulifikia Jeshi la Polisi lilianza ufuatiliaji na ndipo kwa kushirikiana na Polisi Malawi lilifanikiwa kukamata Bajaji hiyo huko nchini Malawi.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kushirikiana na Polisi Malawi na Polisi wa Kimataifa kumtafuta mtu mmoja anayedaiwa kununua Bajaji kutoka Tanzania pamoja na mtandao mzima unaojihusishaji na wizi wa vyombo hivyo vya moto [Bajaji na Pikipiki].

KUPATIKANA NA BHANGI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa 1. JOSEPH KOMBWE [31] Mkazi wa Isyesye na 2. OSCAR JOHN [31] Mkazi wa Ilemi kwa tuhuma ya kupatikana na dawa za kulevya aina ya Bhangi Gramu 30.

Watuhumiwa walikamatwa mnamo tarehe 20.05.2021 majira ya saa 02:30 usiku huko Mtaa wa Juhudi, Kata ya Ilemi, Tarafa ya Sisimba, Jijini Mbeya. Watuhumiwa ni watumiaji wa Bhangi. Upelelezi unaendelea.

KUPATIKANA NA BHANGI PAMOJA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia JOHN JOHN MWALUSELE [38] Mkazi wa Kyela kwa tuhuma ya kupatikana na dawa za kulevya aina ya Bhangi Gramu 25 kwenye kibanda chake cha biashara.

Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 20.05.2021 majira ya saa 13:55 mchana huko eneo na Kata ya Mbugani, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya.

Katika upekuzi uliofanywa katika kibanda hicho, mtuhumiwa alikutwa na pombe kali zilizopigwa marufuku nchini tokea nchini Malawi aina ya Ice London Gin, Raider na Coffee katoni 03. Upelelezi unaendelea.

Post a Comment

0 Comments