BRELA yawapa somo Wabunifu kusajili vumbuzi zao

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) imewapa mafunzo wabunifu wanaoshiriki mashindano ya Kiitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) yanayoendelea katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Afisa Mwandamizi-Utumishi na Utawala kutoka Idara ya Miliki Ubunifu BRELA, Bw Raphael Mtalima akitoa mada juu ya sifa za Uvumbuzi unaoweza kusajiliwa kama Hataza kupitia BRELA wakati wa semina kwa Wabunifu katika mashindano ya MAKISATU yanayofanyika katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo. BRELA inawakaribisha kutembelea kwenye banda lake katika mashindano ya MAKISATU yaliyoanza tarehe 6 hadi 11 Mei, 2021

Akizungumza katika mafunzo hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Jijini hapa, Afisa Utumishi na Utawala anayehusika na uchambuzi wa Hataza, Alama za Biashara Raphael Mtalima alisema mvumbuzi lazima alinde Ubunifu wake kisheria.

"Tuko hapa kutoa elimu kwa wabunifu wetu 70 ambao wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania ushindi wa MAKISATU mwaka huu,lengo ni kutaka wabunifu walinde bunifu zao kisheria", alisema Mtalima.
Baadhi ya Wabunifu wakifuatilia elimu inayotolewa na Afisa Mwandamizi- Utumishi na Utawala kutoka Idara ya Miliki Ubunifu BRELA, Bw Raphael Mtalima juu ya sifa za Uvumbuzi unaoweza kusajiliwa kama Hataza kupitia BRELA wakati wa Semina kwa Wabunifu katika mashindano ya MAKISATU yanayofanyika katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo. BRELA inawakaribisha kutembelea kwenye banda lake katika mashindano ya MAKISATU yaliyoanza tarehe 6 hadi 11 Mei, 2021.

Mtalima alisema wabunifu wamekuwa wakitumia gharama kubwa kutengeneza Bunifu zao hivyo wana kila sababu ya kulinda bidhaa zao kisheria kwa kusajili bunifu zao Brela.

"Kuna watu wapo kwa ajili ya kuangalia nani kafanya nini,akiona kitu kimebuniwa kizuri, anacopy na kupest na baadae anajimilikisha kisheria kwa kufanya Usajili na kuwa na hakimiliki", alisema Afisa huyo.
Mashindano ya MAKISATU yanayoenda sambamba na maonesho ya Wabunifu yalianza Mei 6 mwaka huu yanatarajiwa kumalizika Mei 11 ambapo Waziri Mkuu anatarajia kuyafunga maonesho hayo.

Aidha Mtalima aliwaambia wabunifu hao wakisajili Bunifu zao zitawasaidia katika Mambo mengi ndani na nje ya Nchi,yaani atatambulika popote atakapokwenda na itaweza kumfaidisha yeye na Taifa pia.

Mmoja wa Wabunifu waliokuwepo katika mafunzo hayo Emmanuel Matola ambaye amebuni mfumo rahisi wa kufundishia ufundi wa Magari alisema mafunzo hayo waliyopata yatawasaidia kupata Ulinzi wa bidhaa zao.

"Unajua wabunifu wengi wa hapa nchini hawana Utamaduni wa kusajili bunifu zao Brela ,hivyo Mara nyingi huikuta wakikosa haki zao inapotokea mtu kaiba bunifu wa mtu mwingine", alisema Matola.

Naye Martha Machumu ambaye ni mbunifu mwanafunzi wa Kidato Cha Sita katika Shule ya Sekondari Ngaza iliyopo Jijini Mwanza alisema amefurahi kupata Elimu hiyo ambayo anaamini itamsaidia katika shughuri zake za kibunifu.

Brela iko katika viwanja vya Jamhuri wakitoa Elimu kwa wabunifu walioshiriki mashindano hayo ili waweze kujitambua na kuthamini kazi zao kwa kuziwekea Ulinzi.

Post a Comment

0 Comments